Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Profesa Makame Mbarawa (wa pili kushoto), akipata maelezo kutoka kwa Mtaalamu
(kushoto) namna ya Kichwa cha Treni kinavyofanya kazi wakati alipokuwa akikagua
kichwa hicho jijini Dar es Salaam.
Aidha, Profesa Mbarawa
ametoa wito kwa wafanyakazi wa Mamlaka hiyo kufanya kazi kwa moyo na kwa
ufanisi ili kuweza kufufua Mamlaka hiyo ambapo kwa kipindi kirefu ilikuwa na
misukosuko mingi.
Naye Meneja wa TAZARA
mkoa wa Tanzania Bw. Fuad Abdallah, amemuhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa Mamlaka
hiyo itaendelea na huduma za usafirishaji wa mizigo na abiria ndani na nje ya
nchi.
“Kwa sasa TAZARA
inaendelea kuboresha na kuimarisha huduma za usafirishaji wa mizigo kutoka
Bandari ya Dar es salaam hadi New Kapiri Mposhi kati ya siku nne hadi saba
ukilinganisha na siku zilizopita”, amesema Bw. Fuad.
Kichwa hicho cha Treni
kimekarabatiwa kwa gharama ya shilingi Bilioni moja ambapo Serikali imeokoa
Bilioni Tisa mpaka Kumi endapo ingenunua kichwa kipya.
|
Post a Comment