Naibu waziri Ofisi ya rais, Tamisemi, Selemani Jafo, akizungumza katika harambe ya kuchangia madawati mkoani Geita, ambayo alikuwa akimwakilisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Akiwa njiani kuelekea Geita mjini, Jafo alipita Jimbo la Busanda wilaya ya Geita Vijijini na Kukagua Mradi wa Maji uliokamilika Kijijini Makondeko kisha Safari ikaelekea Kijiji cha Chankorongo ambapo kuna Mradi wa Maji wa muda mrefu usio kamilika ambapo mpaka sasa umetumia zaidi ya Bilioni moja na dalili za kukamilika bado.
Kufuatia hali hiyo, Naibu Waziri huyo amemwagiza Katibu tawala wa Mkoa wa Geita Selestine Gesimba kuunda tume maalum ya kuchunguza sakata la mradi huo wa maji wa Chankorongo ambapo wamepewa mwezi mmoja kukamilisha uchunguzi huo.
Alimwagiza Katibu Tawala Mkoa akishirikiana na Wakurugenzi wote kuhakikisha suara la Oprass linapewa kipaumbele kwa watumishi na linafanyika kwa wakati na ipasavyo.
Naibu Waziri aliwahakikishia watumishi kuwa serikali inafuatilia changamoto mbalimbali zinazowakabili na kuwataka wawe na Subra.
Wakati huo huo, akiwa Mkoani Geita Jafo alimwakilisha Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa katika Harambee ya ya kuchangia Madawati.
Katika harambe hiyo Jafo alihamasisha na kuweza kukusanywa kiasi cha Shilingi Bilioni Moja, mia saba arobaini Milioni , laki tano na elfu tisini na saba (1,740,597,000) Kiasi ambacho kilimfanya Mkuu wa Mkoa huo Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga kumshukuru sana Naibu waziri huyo kwani hakutegemea kiasi hicho kikubwa cha Fedha kuweza kupatikana.
|
Post a Comment