Rais wa Umoja wa Waandishi wa Riwaya wenye Dira Tanzania (UWARIDI) Bw. Hussein Tuwa akitoa neno wakati wa uzinduzi wa Umoja huo katika ukumbi wa Nafasi Arts Space Jijini Dar es Salaam.
“Katika azma ya kukuza na kuendeleza Lugha ya Kiswahili tuige mfano wa Rais wetu Mhe.Dkt John Pombe Magufuli wa kutumia Lugha ya kiswahili katika hotuba zake mbalimbali za kitaifa na kimataifa” alisema Bibi. Hajjat Shani.
Kwa upande wake mmoja ya wajumbe wa kamati kuu Bi. Matilda Sendwa katika risala yao kwa mgeni rasmi amesema kuwa Umoja wa Waandishi wa Riwaya wenye Dira Tanzania(UWARIDI) wameamua kutafuta njia ya kurudisha, kutetea, kulinda na kuipandisha heshima yetu kama waandishi na heshima ya kazi zetu zote.
“Tumeamua kutafuta mbinu za kuweza kuhakikisha kuwa heshima ya kazi zetu zinatambuliwa rasmi kiserikali na kijamii kwa ujumla kwa kuanzisha umoja wetu ambao utakuwa na sauti katika kutetea haki za waandishi na kazi zao alisisitiza Bi. Matilda.
Umoja wa Waandishi wa Riwaya wenye Dira Tanzania (UWARIDI) umeanzishwa kwa lengo la kuwatetea waandishi wa Riwaya nchini ili waweze kunufaika na kazi zao.
|
Post a Comment