Mwenyekiti
wa Chama cha United Democratic Party
(UDP) John Momose Cheyo akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani)
kuhusu hali ya kisiasa nchini katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara
ya Habari – Maelezo leo Jijini Dar es Salaam, Kutoka kushoto ni Mkurugenzi
Msaidizi wa Idara ya Habari – Maelezo Tiganya Vicent na Kaimu Katibu Mkuu wa
Chama hicho Goodlucky Ole Medeye.
Aliongeza kuwa Jeshi la Polisi linapotoa katazo la
maandamano ni lazima utii uwepo, kwani Polisi wapo kwa mujibu wa Sheria na Katiba. Ikiwa Chama hicho hakikuridhika na
katazo hilo basi wanatakiwa kuonana na Waziri anayehusika na Jeshi la Polisi.
Akifafanua zaidi alisema kuwa Rais Magufuli amekuwa
akichukua hatua za makusudi za kutatua
matatizo mbalimbali kama vile kupambana na ufisadi, ambapo viongozi wengi wa
Serikali wamesimamishwa kazi au kufukuzwa kutokana na kujihusisha na masuala ya rushwa.
Mwenyekiti huyo wa UDP amewataka watanzania kumuunga mkono Mhe.
Rais Magufuli ili aweze kutimiza ndoto zake na yale ambayo ameyaahidi kwa ajili
ya nchi ya Tanzania.
Aidha Cheyo aliwasifu viongozi wa Dini ambao walikaa na Viongozi
wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) na kukubali kurudi bungeni bila pingamizi
lolote. Amewataka viongozi hao wa dini kuendelea kuzungumzia suala la amani kwa
Watanzania na Viongozi wa kiasa ili kudumisha amani ya nchi.
|
Post a Comment