Serikali Mkoani SIMIYU yatoa Ufafanuzi Suala la Walimu Wakuu Kuvuliwa Madaraka
Na Stella Kalinga, Simiyu
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka ametoa ufafanuzi wa agizo la kufanya mabadiliko ya Walimu wakuu, Wakuu wa Shule na Waratibu Elimu Kata mkoani humo, ambalo Serikali ya Mkoa ililitoa tarehe 17 Agosti ,2016 katika kikao ambacho alipokea Vishikwambi (tablets) 637 kutoka EQUIP Tanzania (Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Nchini) kwa ajili ya Walimu wakuu na Waratibu wa Elimu Kata
Mkuu huyo wa Mkoa ametoa ufafanuzi huo kufuatia kuwepo kwa taarifa za upotoshaji wa agizo hilo kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii., kuwa Mkuu wa Mkoa ametangaza kuwavua madaraka Walimu wakuu, Wakuu wa Shule na Waratibu Elimu Kata wote wa Mkoa huo; hali iliyopelekea baadhi ya Walimu wakuu na Waratibu kukosa ari ya kufanya kazi, kwa kigezo cha kusubiri kuvuliwa madaraka.
Mtaka amesema Mkoa ulipokea taarifa za takwimu za wanafunzi hewa, vyumba vya madarasa, idadi ya walimu na idadi ya madawati, baada ya kupokea taarifa hizo ulionekana utofauti mkubwa wa takwimu hizo ndipo Serikali mkoani humo, ikaahidi kupitia mapungufu ya udanganyifu wa takwimu hizo kwa kila shule na kuchukua hatua ikiwa ni pamoja na kuwawajibisha Walimu wakuu na Wakuu wa Shule waliodanganya idadi ya wanafunzi.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthon Mtaka akizungumza na Maafisa Elimu na Viongozi
wa CWT wa Mkoa huo katika kikao maalum cha kutoa ufafanuzi wa agizo
lililotolewwa na Serikali Mkoani humo la kufanya mabadiliko ya Walimu wakuu na
Waratibu Elimu kata, ambalo liliripotiwa tofauti katika vyombo ya habari na
mitandao ya kijamii. kuwa Serikali imetangaza kuwavua madaraka.
Baadhi ya Wajumbe wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu (hayupo pichani) katika kikao maalum cha kutoa ufafanuzi wa agizo
lililotolewa na Serikali Mkoani humo la kufanya mabadiliko ya Walimu wakuu na
Waratibu Elimu kata, ambalo liliripotiwa tofauti katika vyombo ya habari na
mitandao ya kijamii. kuwa Serikali imetangaza kuwavua madaraka.
Aidha, Mtaka amesema Mkoa wa Simiyu umepata bahati ya kuwa na Mradi wa EQUIP Tanzania ambao umewawezesha waratibu kupata pikipiki na posho, walimu wakuu wamepewa vishikwambi kwaa jili ya utunzaji wa takwimu, hivyo Serikali inao wajibu wa kuangalia mahitaji ya Mkoa katika elimu ambapo alielekeza yafanyike mabadiliko ya Walimu wakuu Msingi, Sekondari na Waratibu wa mkoa mzima.
“Nililisema mwanzo na leo nalirudia tutafanya mabadiliko makubwa kwa Wakuu wa Shule za Msingi, Sekondari na Waratibu Elimu kata kwa kujiridhisha na maendeleo ya shule zetu, idadi ya walimu waliopo,idadi ya wanafunzi, kiwango cha ufaulu wa wanafunzi na mazingira ya shule ; lakini tutatoa upendeleo kwa shule 10 bora katika kila wilaya kwa Mitihani ya Kitaifa ya Darasa la IV, VII Kidato cha II na IV , hiki ni kipimo kimojawapo cha walimu wa kuendelea nao. Nasisitiza hakuna mtu atakayeonewa wala kufedheheshwa”, alisema Mtaka.
Mtaka amesema azma ya Serikali ni kuibua vipaji vipya vya viongozi wa Elimu katika ngazi ya Wilaya ambapo alisema ameshaagiza Maafisa Elimu wa Wilaya kuwasilisha taarifa ya walimu waliojiendeleza katika ngazi shahada ya kwanza na shahada ya uzamili ili watakaokuwa na sifa waweze kuteuliwa katika nafasi za Walimu wakuu, Wakuu wa Shule na Waratibu Elimu Kata ambao watafanyiwa upekuzi (vetting) na Vyombo vya Ulinzi na Usalama.
Katibu wa CWT Mkoa wa Simiyu, Said
Mselema(kulia) akizungumza na Maafisa
Elimu na Viongozi wa CWT wa Mkoa huo (hawapo pichani) katika kikao maalum cha
kutoa ufafanuzi wa agizo lililotolewa na Serikali Mkoani humo la kufanya
mabadiliko ya Walimu wakuu na Waratibu Elimu kata, ambalo liliripotiwa tofauti
katika vyombo ya habari na mitandao ya kijamii, kuwa Serikali imetangaza
kuwavua madaraka.
Baadhi ya Wajumbe wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu (hayupo pichani) wa kikao maalum
cha kutoa ufafanuzi wa agizo lililotolewwa na Serikali Mkoani humo la kufanya
mabadiliko ya Walimu wakuu na Waratibu Elimu kata, ambalo liliripotiwa tofauti
katika vyombo ya habari na mitandao ya kijamii. kuwa Serikali imetangaza
kuwavua madaraka.
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini
akizungumza na Maafisa Elimu na Viongozi wa CWT wa Mkoa huo (hawapo pichani)
katika kikao maalum cha kutoa ufafanuzi wa agizo lililotolewa na Serikali
Mkoani humo la kufanya mabadiliko ya Walimu wakuu na Waratibu Elimu kata,
ambalo liliripotiwa tofauti katika vyombo ya habari na mitandao ya kijamii,
kuwa Serikali imetangaza kuwavua madaraka.
Sanjari na hilo ,
Mkuu huyo wa Mkoa amesema Walimu wakuu na Wakuu wa shule wa zamani ni tofauti
na wale wa sasa, kwa kuwa sasa hivi
wamekuwa maafisa masuuli wa shule zao ambapo wanapokea fedha za Elimu bila
malipo kupitia akaunti za shule zao, hivyo ni lazima wapatikane watu waadilifu,
wenye sifa na uwezo wa kuongoza shule na kusimamia fedha za Serikali.
Akichangia
katika kikao hicho Afisa Elimu (Msingi) Wilaya
ya Meatu, George Lowasa ameshauri Uchambuzi wa watu watakaoteuliwa ufanyike katika
umakini mkubwa ili wapatikane watendaji wazuri na kuhusu utoaji wa takwimu
sahihi alishauri kuwe na utaratibu wa kuziboresha kila (robo) baada ya miezi
mitatu ili kuwa na takwimu sahihi pale zinapohitajika.
Kwa upande wake
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini amesema Uteuzi huo utazingatia
sheria, kanuni, taratibu na miongozo ya uteuzi ambapo hakuna mtu atakayeonewa au
atakayependelewa.
Wakati huo huo Mkuu
wa Mkoa amesema atawachukulia hatua Maafisa wale wanaolalamikiwa na walimu kwa
kuwatolea lugha mbaya kila wanapotoa
huduma kwa walimu hao katika Halmashauri za Mkoa huo.
Naye Katibu wa
CWT Mkoa wa Simiyu, Said Mselema ameshauri baada ya mabadiliko ya wakuu wa shule na
Waratibu wa Elimu Kata kufanyika wale ambao wataonekana hawana sifa za
kuendelea kushika nafasi hizo waondolewe kwa staha, ambapo aliomba Serikali
ngazi ya Wilaya na Mkoa ikishirikishe chama hicho katika masuala yote muhimu ya
kuendeleza sekta ya Elimu, kwa kuwa wanamsaidia mwajiri katika usimamizi wa
utendaji kwa walimu.
Kikao hicho cha
wadau kilichofanyika mjini Bariadi na kimewahusisha
Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa, Maafisa Elimu kutoka
Halmashauri zote za Mkoa wa Simiyu
pamoja na Wenyeviti na Makatibu wa Chama
cha Walimu Tanzania (CWT) ngazi ya Mkoa
na Wilaya.
Post a Comment