Walemavu 19 Watunukiwa Vyeti vya Udereva Jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Usalama Barabarani Wilaya ya Ilala, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP), Peter Mashishanga (kulia), akimkabidhi cheti, Mpoki Mwasunga, baada ya kuhitimu mafunzo ya udereva ya mwezi mmoja katika chuo cha udereva cha Nyato's kilichopo Majohe Bomba mbili Manispaa ya Ilala Dar es Salaam leo. Wahitimu 19 ambao ni walemavu walihitimu mafunzo hayo.
Mkurugenzi wa shule hiyo Wilfred Nyato (kulia), akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mkuu wa Usalama Barabarani Wilaya ya Ilala, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP), Peter Mashishanga, akiangalia alama ya usalama barabarani. Kushoto ni Mwenyekiti wa Taifa wa Kamati ya Taifa ya Usalama Barabarani kwa watu Wenye Ulemavu, Kabateke Jutoram na Mkurugenzi wakitengo cha Elimu kwa Umma kikosi cha Usalama barabarani nchini,Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP),Mossi Ndozero.
Wahitimu wakiwa kwenye hafla hiyo.
Mshairi, Kiiza Amani akitoa burudani kwenye hafla hiyo.
Mkuu wa Usalama Barabarani Wilaya ya Ilala, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP), Peter Mashishanga (katikati), akihutubia kwenye hafla hiyo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Taifa wa Kamati ya Taifa ya Usalama Barabarani kwa watu Wenye Ulemavu, Kabateke Jutoram na Mkurugenzi wakitengo cha Elimu kwa Umma kikosi cha Usalama barabarani nchini,Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP),Mossi Ndozero.Mkurugenzi wakitengo cha Elimu kwa Umma kikosi cha Usalama barabarani nchini,Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP),Mossi Ndozero, akitoa neno kwenye mkutano huo.
Hapa James Hizza akipokea cheti chake.
Sikujua Mbwembwe, akikabidhiwa cheti chake.
Wahitimu wakionesha vyeti vyao.
Stafu Sajeni, Enock Machunde akitoa darasa kwa hitimu hao kuhusu sheria za usalama barabarani.
Koplo, Faustina Ndunguru, akizungumza kwenye mkutano huo.
Na Dotto Mwaibale
WATU Jamii ya walemavu ambao ni maderava wa vyombo vya moto wametakiwa kujitokeza kwenye shule mbalimbali za udereva ili kupata mafunzo ya udereva ikiwa pamoja na kupata leseni kabla ya kutumia vyombo hivyo.
Wito huo umetolewa Dar es Salaam leo na Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa kipolisi wa Ilala,Peter Mashishanga wakati akiwatunuku vyeti walemavu 19 ambao wa mefunzo ya mwenzi mmoja katika shule ya udereva ya Nyato's iliyopo Majohe Bomba mbili Manispaa ya Ilala.
Alisema kuwa ipo haja ya walemavu ambao wanamiliki vyombo vya moto na kuendesha vyombo hivyo kabla hawajaingia barabarani ni vema wakapata mafunzo ya kujuwa alama,kanuni na sheria za usalama barabarani.
"Ni muhimu kwa kundi hili ambalo leo mmepata vyeti vya kuhitimu mafunzo ya udereva kwenda kuwa mabalozi kwa wengine ambao hawajapata fursa ya kupata mafunzo kama nyie kwenda kuwahamasisha ili wajiunge katika vyuo vya udereva ikiwamo chuo hiki cha Nyato's ambacho kimeaza mpango wa kutoa mafunzo haya kwa nchi nzima kwa kushirikiana Kamati ya Taifa ya Usalama Barabarani kwa watu Wenye Ulemavu."alisema Mashishanga
Aidha aliwaeleza wahitimu hao kuwa wahakikishe wanakwenda kupata majaribio kwa wa kufunzi wa kikosi cha Usalama barabarani ili wapate leseni zitakazo wafanya waweze kuendesha vyombo vya vya moto.
Kwaupande wake Mkurugenzi wakitengo cha Elimu kwa Umma kikosi cha Usalama barabarani nchini,Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP),Mossi Ndozero alisema kuwa ni muhimu kwa wahitimu hao kwenda kuzingatia sheria za usalama barabarani ikiwa pamoja na kuvaa kofia ngumu,na kutozidisha abiria.
Naye Mkurugenzi wa shule hiyo Wilfred Nyato alishukuru kwa ushirikiano uliopo kati ya Jeshi hilo na taasisi yake ambapo pia ametoa ofa ya kusoma bure kwa mlemavu Thomas Kone ambaye hivi karibuni alipata msaada wa bajaji kutoka kwa Rais Dk. John Magufuli.
Nyato alisema kuwa kimeazisha mpango wa kutoa mafunzo ya udereva kwa kushirikiana na kamati ya Taifa ya usalama kwa watu wenye ulemavu kwa lengo la kukabiliana na matukio ya ajali za barabarani.
Post a Comment