Makamu wa Rais SAMIA SULUHU amuwakilisha Dkt MAGUFULI Swaziland Mkutano wa SADC
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania SAMIA SULUHU HASSAN amewasili mjini Mbabane - Swaziland leo kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa 36 wa Wakuu wa nchi na serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika- SADC-.
Makamu wa Rais SAMIA SULUHU HASSAN atamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Dakta JOHN MAGUFULI katika mkutano huo ambao utafanyika tarehe 29 Agosti 2016 ambapo Tanzania inatarajiwa kukabidhiwa nafasi ya Uenyekiti wa Jumuiya hiyo.
Mkutano huo wa 36 wa SADC ni maalum kwa wakuu wa nchi na serikali wanaounda Kamati ya siasa,ulinzi na usalama ambao watajadili kwa kina hali ya siasa na usalama, demokrasia na maombi ya Burundi na Comoro kwa ajili ya kujiunga na SADC.
Makamu wa Rais SAMIA SULUHU HASSAN katika msafara wake amefuatana na Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Kikanda na Kimataifa Augustine Mahiga, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage na Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Amina Salum Ali.
Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
Mbabane – SWAZILAND.
Post a Comment