Na Theresia Mwami TEMESA
Mafundi wa TEMESA wameshauriwa kutumia mafunzo waliyoyapata kuendana na mabadiliko ya teknolojia katika utengenezaji magari na vifaa vya umeme.
Ushauri huo umetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Mjumbe wa Bodi ya Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Brigedia Jenerali Msataafu Mhandisi Mabula Mashauri wakati wa hafla ya kuhitimisha mafunzo kwa mafundi Wakala hao iliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT).
Brigedia Jenerali Msataafu Mhandisi Mabula Mashauri amesema kuwa Serikali kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA imedhamiria na kuhakikisha kuwa magari na mitambo yote ya Serikali inatengenezwa kitaalam ili kuleta tija na thamani halisi ya fedha iliyokusudiwa pamoja na kukidhi kiu na matarajio ya wateja.
”Napenda kuwakumbusha kwamba mnayo dhamana kubwa ya kutengeneza magari ya Serikali hivyo kwa mafunzo mliyoyapata ninaamini mmejenga uwezo wa kutosha wa kuhudumia magari na vifaa vya umeme kwa kutumia mfumo wa kisasa” alisema Mhandisi Mashauri.
|
Post a Comment