Wajumbe kutoka Serikalini na Asasi za
Kiraia wakimsikiliza Naibu Mwanasheria mkuu wa Serikali Mhe. Gerson Mdemu
wakati wa ufungaji wa kikao kikao kuhusu mapendekezo yaliyotolewa kwa serikali
wakati wa majadiliano ya taarifa ya nchi ya utekelezaji wa masuala ya haki za
binadamu chini ya mfumo wa mapitio kwa kipindi maalum na baraza la haki za
binadamu la umoja wa mataifa, Leo Jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo, Tanzania ilikubali
kutekeleza mapendekezo 130 tu kati
ya 227 yaliyokuwa yanahusu mchakato wa
Katiba,kuijengea uwezo Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, kuhuisha Sera
za nchi ili ziendane na malengo endelevu ya Dunia ,kuandaa taarifa za nchi za
utekelezaji wa masuala ya haki za binadamu na kuziwasilisha kwenye vyombo vya
vya umoja wa mataifa kwa wakati.
Vilevile Serikali iliahirisha jumla ya mapendekezo 25 ambayo
yalijikita katika marekebisho ya sheria
ya Takwimu, 2015, Sheria ya makosa ya mtandao, 2015,ukamilishaji wa Sheria ya
Habari, Sheria ya vyombo vya Habari,uandaaji wa mikakati na mipangokazi ya
utekelezaji wa msuala ya kuzuia ndoa za utotoni na za kulazimishwa ,upitishaji
wa sera mpya mbalimbali ikiwemo ya kutoa vyeti vya kuzaliwa na usajili wake kuwa
bure na masuala ya uchaguzi Zanzibar, kwa lengo la kuyapitia tena kwa kina na
kushirikisha zaidi wadau ili hatimaye kuweka msimamo stahiki kabla mapendekezo
hayo hayajawasilishwa tena Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kwa
hatua za mwisho za kupitisha rasmi taarifa ya nchi katika kukuza na kulinda
haki za Binadamu.
Aidha, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali
ametumia fursa hiyo kusisitiza kuwa
Serikali itaendelea kulinda na kukuza haki za bindamu ikiwa ni pamoja na
kupokea hoja na maoni ya wadau ili kuboresha taarifa ya nchi itakayowasilishwa
katika Baraza la Haki za Binadamu la umoja wa mataifa kabla au ifikapo tarehe 9
Septemba, 2016 na kuwataka watanzania wote kushiriki ipasavyo katika dhana
nzima ya kukuza na kulinda haki za bindamu nchini.
Utaratibu wa Mapitio kwa kipindi
maalum (The Universal Periodic Review) wa masuala ya haki za binadamu
ulianzishwa na Umoja wa Mataifa mnamo mwaka 2006 kwa lengo la kuzifanyia
mapitio nchi 192 ambazo ni wanachama wa Umoja wa Mataifa, Tanzania ikiwa miongoni,
kwa lengo la kuangalia utekelezaji wa masuala ya kulinda na kukuza haki za
binadamu nchini mwao.
Picha na Hassan Silayo-MAELEZO
|
Post a Comment