Vituo vya Afya Jijini TANGA vinatakiwa Kusaidiwa Ili Kuiondolea Mzigo Hospitali ya BOMBO
Mganga Mku wa Mkoa wa Tanga (RMO)
Dkt Asha Mahita akisisitiza jambo wakati akizungumza na Mbunge wa Jimbo
la Tanga (CUF) ambaye alikwenda kuitembelea hospitali ya Mkoa wa Tanga
Bombo kuangalia changamoto zinazowakabili.
Ombi hilo lilitolewa jana na Mganga Mku wa Mkoa wa Tanga (RMO) Asha Mahita wakati Mbunge huyo alipoitembelea hospitali ya alisema kuwa msongamano unaoikabili Hospitali ya Rufaa ya Mkoa unatokana na kutokuwepo na ubora katika zahanati na vituo vya afya jambo ambalo linalowafanya wanachi kukimbilia katika Hosptiali hiyo.
Hatua hiyo inatokana na zahanati na vituo vya afya vingi Jijini Tanga kukakabiliwa na changamito nyingi zinazo sababisha kukosa ubora hali inayochangia kwa asilimia kubwa wananchi wengi kukimbilia katika hospital ya Rufaa ya Bombo na kuongeza msongamano wa wagonjwa.
Mahita alisema ipo haja ya kuvisaidia vituo hivyo ambavyo havina nyumba za watumishi, uzio, miundombinu mibovu na vingine kukosa umeme jambo ambalo linakuwa si rafiki kwa wahudumu na linakwamisha shughuli za kiafya hasa nyakati za usiku.
Mbunge wa Jimbo la Tanga
(CUF) Mussa Mbaruku akisisitiza jambo kwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga
(RMO) Dkt Asha Mahita.
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF)
Mussa Mbaruku katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na madaktari kutoka
katika taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya The Sunshine Muslim
Volunteer huku wakishirikiana na madaktari bingwa kutoka nchi za
Uingereza,
Afrika kusini, Canada na Pakistani waliokuja kuweka kambi ya siku tano
kwa
ajili ya kutoa matibabu bure ya Fistula.
Alisema kuwa iwapo kutakuwepo na mabororesho katika vituo hivyo huku Serikali na wadau mbalimbali wakiweka nguvu zao katika swala la kumalizia Hospitali ya wilaya ambayo mpaka sasa inajengo moja la ghorofa kwa ajili ya utawala ikimaliziwa na kuanza kutumika kutapunguza kwa asilimia kubwa msongamano kwenye hospitali hiyo.
Kwa upande wake, Mbunge Mussa Mbaruku alihaidia kuangalia namna ya kuzipatia ufumbuzi changamoto hizo kwani wananchi afya zao zinapokuwa zimeimarika inawasaidia kuweza kufanya shughuli za kujiingizia kipato.
“Ndugu zangu huu si muda wa kupiga porojo kuhusiana na masuala ya afya ambalo ndio uti wa mgongo wa wananchi hivyo lazima viongozi wajenge umoja na kutafuta njia ya kuweza kuviboresha vituo hivyo ambavyo vitawasaidia kwa asilimia kubwa wananchi kupata huduma hiyo kwa ukaribu zaidi “Alisema.
Aidha alisema pamoja na changamoto zinazozikabili zahanati na vituo hivyo lazima Serikali itenge fedha za kutosha ili kuweza kuimalizia Hospitali ya Wilaya iliyopo Masiwani Shamba ambayo mpaka sasa bado hakuna majibu sahihi ya kukwama kwa umaliziwaji wa Hosptili hiyo.
MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CUF),
Mussa Mbaruku ameombwa kuangalia namna ya
kuweka mkakati wa kuvisaidia vituo vya afya na Zahanati zilivyopo ndani ya Jiji
la Tanga ili kupunguza msongamano wa wagonjwa katika Hospitali ya mkoa wa Tanga
Bombo inayohudumia wagonjwa wa mkoa mzima.
“Bado nashindwa kupa majibu ni
kitu gani kinachokwamisha kumalizika kwa
Hospitali ya Wilaya ambayo tayari inajengo zuri la utawala tena la ghorofa
serikali inawajibu kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha Hospitali
hiyo inamalizika na inakuwa na kiwango bora katika sekta zote za
matibabu.
Mbaruku alifanya mazungumzo
hayo na mganga mkuu wa Mkoa alipo watembelea
madaktari kutoka katika taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya The Sunshine Muslim
Volunteer huku wakishirikiana na madaktari bingwa kutoka nchi za Uingereza,
Afrika kusini, Canada na Pakistani waliokuja kuweka kambi ya siku tano kwa
ajili ya kutoa matibabu bure ya Fistula.
Post a Comment