Katibu Mkuu wa Wizara
ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga, amekagua na kuridhika
na hatua ya ujenzi na ukarabati wa vivuko vitatu na tishari moja unaoendelea
Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza mara baada
ya kukagua ukarabati wa kivuko cha MV Magogoni, MV Tanga, New MV Magogoni na Tishari
litakalotumiwa na Kivuko cha MV Dar es Salaam Eng. Nyamhanga amewapongeza
mafundi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) na kampuni ya M/S Songoro Marine
Transport Boat Yard Ltd kwa kufanya kazi kwa kasi na ubora unaotakiwa.
“kazi yenu ya ujenzi
na ukarabati wa kivuko cha MV Magogoni, MV Tanga, Kivuko kipya cha Magogoni na
Tishari inafanyika kwa viwango vinavyokubalika na hivyo baadae mwezi huu,
vivuko vya MV Tanga na MV Magogoni vitaanza kazi, Hongereni”, amesema Eng. Nyamhanga.
|
Katibu Mkuu Wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga
akikagua michoro ya vivuko vitatu na Tishari Moja ambavyo ujenzi wake upo
katika hatua za mwisho za kukamilika jijini Dar es Salaam, katikati ni Kaimu
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Eng. Manase Ole Kujan.
|
Post a Comment