WAFUGAJI KANDA YA ZIWA WALALAMIKA KWA KATIBU MKUU WA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM, KOMREDI ABDULRAHMAN KINANA
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akilakiwa na Katibu wa CCM mkoa wa Kagera Bw. Ali Ame wakati alipowasili katika kata ya Nyakanazi wilayani Biharamulo mkoani Kagera wakati akianza rasmi ziara yake ya kikazi ya kukagua na kuhimiza utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 inayotekelezwa na serikali.
Ziara hiyo itafanyika katika mikoa mitatu ya kanda ya ziwa ambayo ni Kagera yenewe, mkoa wa Geita na kisha atamalizia na mkoa wa Mwanza kwa kufanya mkutano mkubwa wa kuhitimisha ziara kutembelea nchi zima ikiwani mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar na majimbo yote ya uchaguzi nchi nzima, ambapo amekutana na wananchi na kusikiliza kero mbalimbali za wananchi, kuzifuatilia na kuzipatia ufumbuzi.
Wakizungumza katika mkutano wafugaji wa kanda ya Ziwa wamelalamikia wizara ya Maliasili na Utalii hasa askari wa wanyamapori ambapo wamesema wamekuwa wakikamata mifugo yao na kuwatoza faini kuanzia shilingi laki mbili mpaka milioni kumi, Mbaya zaidi wanapodai haki yao wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya kikatili kupita kiasi jambo ambalo linawakatisha tamaa ya maisha kabisa.
Wafugaji hao wameongeza kwamba vikao mbalimbali vimeshafanyika zaidi ya 17 kupitia ngazi zote za kitaifa kasoro kwa Mh. Rais tu ndiyo hatujafika, lakini vikao hivyo vyote havijazaa matunda.
bado hali ni mbaya na manyanyaso yanazidi kuendelea, wamemuomba Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kuwasaidia ili waweze kupata ufumbuzi wa suala hilo na wao waweze kuishi na kufanya shughuli zao kwa amani.
Katika ziara zake hizo Kinana amekuwa akiongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa CCM Ndugu Nape Nnauye.
(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-KAGERA)
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM wakisalimiana na viongozi mbalimbali mara baada ya kulakiwa katika kata ya Nyakanazi Wilayani Biharamulo leo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akivishwa skafu mara baada ya kulakiwa katika kata ya Nyakanazi Wilayani Biharamulo leo.
Baadhi ya viongozi wakifurahia ujio wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana mara baada ya kulakiwa katika kata ya Nyakanazi Wilayani Biharamulo leo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na viongozi mbalimbali na wananchi mara baada ya kulakiwa katika kata ya Nyakanazi Wilayani Biharamulo leo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Nape Nnauye wakisalimiana na wananchi mbalimbali mara baada ya kulakiwa katika kata ya Nyakanazi Wilayani Biharamulo leo.
Mtoto akiwa amembeba mtoto mwenzake wakati wa mapokezi hayo
Ali Ame katika wa CCM mkoa wa Kagera akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi mbalimbali mara baada ya kulakiwa katika kata ya Nyakanazi Wilayani Biharamulo leo.
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza Kinana mara baada ya kumpokea katika mji wa Nyakanazi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Mwenyekiti wa Chama cha Wafugaji Kanda ya Ziwa Bwa.Mugisha Mushad wakati alipokuwa akitoa malalamiko ya wafugaji kwa ukatili wanaofanyiwa na askari wa wanyamapori katika mapori mbalimbali ya hifadhi kanda ya ziwa.
Baadhi ya wafugaji wakimsiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana hayupo pichani wakati alipokuwa akizungumza nao katika mji wa Nyakanazi.
Katibu Msaidizi Chama cha Wafugaji Kanda ya Ziwa Bwa. Khamis Biteko akitoa ushuhuda wa manbo wanayofanyiwa wafugaji hao na askari wa wanyamapori wakati wa mkutano huo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wafugaji wa Kanda ya Ziwa wakati walipokutana naye katika mji wa Nyakanazi wilayani Biharamulo na kutoa kero zao kwake juu ya manyanyaso wanayofanyiwa na askari wa wanyamapori.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Mwenyekiti wa Chama cha Wafugaji Kanda ya Ziwa Bwa.Mugisha Mushad wakati alipokuwa akinuobyesha eneo linalotumika kuhifadhi mifugo yao mara inapokamatwa eneo hilo ni dogo na halina chakula cha mifugo wala maji jambo ambalo linafanya mifugo kufa kwa wingi ikiwa imekamatwa.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyeshwa eneo hilo na wananchi mbalimbali wakati alipotembelea na kujionea eneo hilo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akielekea kuwasalimia wananchi wa katika kijiji cha Kyamyorwa.
Nape Nnauye akizungumza na wananchi katika kijiji cha Kyamyorwa wakati msafara wa Katibu Mkuu uliposimama kuwasalimia wananchi hao.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akilimiana na wananchi wa kijiji cha Kyamyorwa .
John Mongela mkuu wa mkoa wa Kagera akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Kyamyorwa.
Post a Comment