Header Ads

Waziri JAFO aagiza Utunzwaji wa Miundombinu ya Shule ya Chang'ombe Manispaa ya Dodoma


Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Seleman Jafo akitoa agizo kwa halmashauri, kamati za shule na mikoa nchini kuacha kufanya kazi kwa mazoea na badala yake kutumia juhudi na maarifa ili kuwaletea wananchi maendeleo kwa haraka. Ameridhishwa na ubora na kasi waliyoitumia kujenga majengo hayo.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Seleman Jafo akifungua mlango ili kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa ambao umekamilika kwa asilimia mia moja.

Mojawapo ya madarasa yaliyokamilika katika shule ya msingi Chang’ombe A Manispaa ya Dodoma. Jumla ya vyumba vya madarasa sita vimejengwa ili kukabiliana na changamoto ya vyumba vya madarasa katika shule hiyo inayotokana na wingi wa wanafunzi, shule hiyo ina zaidi ya wanafunzi 2000.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Seleman Jafo akizungumza na walimu, wanafunzi na Kamati ya shule ya msingi Chang’ombe A Manispaa ya Dodoma alipofanya ziara kujionea maendeleo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ambao umekamilka kwa asilimia mia moja, Kulia kwake ni Kaimu Afisa Elimu Mkoa Dodoma Tumsifu Mwasamale na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo  Nelly kinyaga kushoto kwake ni Diwani Kata ya Chang’ombe Mhe.Bakari Samweli Fundikira.
...............................................

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na  Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Seleman Jafo amewataka wanafunzi na walimu wa shule ya msingi ya Chang’ombe  kutunza   na kuitumia  miundombinu iliyojengwa ili kuongeza ufaulu katika shule hiyo.

Jafo ametoa kauli hiyo leo alipotembelea shule hiyo ili kukagua utekelezaji wa agizo  alilolitoa juu ya kukamilisha ukarabati wa miundombinu  katika  shule hiyo  ifikapo 10 januari, mwaka huu.

Novemba 3, mwaka jana Jafo alitoa agizo kwa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma kuhakikisha inakamilisha ujenzi wa matundu 20 ya vyoo na vyumba vya  madarasa 8 pamoja  na ukarabati wa vyumba vya madarasa  2 katika shule ya Chan’gombe A  ifikapo januari, 10 mwaka huu kabla ya msimu wa masomo kuanza.

 Katika ziara hiyo, Jafo amesema ameridhishwa  kwa  hatua nzuri  ya  ukarabati huo na kupongeza  uongozi wa Halmashauri ya  Manispaa , kamati ya shule ya Chang’ombe ,walimu na Diwani wa Kata ya Chang’ombe kwa utekelezaji huo.

Amesema shule hiyo inapaswa kuongeza ufaulu wake ili iwe mfano mzuri wa kuigwa kwa shule nyingine .

Amebainisha awali alitoa agizo hilo baada ya kubaini changamoto mbalimbali katika shule ya msingi ya Chang’ombe A .

 ‘’Maagizo niliyoyatoa yalikuwa magumu sana lakini nia yangu ilikuwa kuwatengenezea mazingira rafiki  wanafunzi na walimu   , nimefarijika na utekelezaji wake, hali haikua nzuri hapo mwanzo lakini nimefarijika kwa  kazi nzuri, muonekano wa madarasa unaridhisha  nawapongeza sana’’  amesema Naibu Waziri huyo

 Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Nelly  Kinyaga  ameishukuru serikali kwa kuboresha miundombinu ya shule  hiyo  ambapo awali mazingira ya shule hiyo yalikuwa sio  rafiki kwa wanafunzi na walimu  kutokana na  upungufu wa matundu 20 ya vyoo na  vyumba vya madarasa 8.

‘’Kwakweli kulikuwa na changamoto sana wanafunzi walikua wengi na madarasa machache  lakini kwasasa hatuna watoto wanaokaa chini na msongamano wa wanafunzi darasani umepungua kwa kiasi kikubwa  ,naishukuru serikali na Jafo kwa kutilia mkazo  ukarabati wa miundombinu ya shule yetu’’ amesema

Mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo, Ally Mohamed Swalehe ameishukuru serikali kwa kuboresha miundombinu ya shule hiyo rafiki  kwa kuwa itaongeza ufaulu katika mitihani  na kuepusha magonjwa ya  milipuko shuleni hapo.

No comments

Powered by Blogger.