Mbunge wa Isimani WILLIAM LUKUVI akabidhi Mabati na Power Tila Kwa Madiwani Wake
Diwani wa Mlolo Charles Nyagawa kushoto akikabidhiwa bati na katibu wa mbunge wa Isimani Thom Malenga. |
Madiwani wakipokea bati. |
MBUNGE
wa jimbo la Isimani Wiliam Lukuvi aametoa msaada wa bati 2000
ajili ya kukamilisha miradi ya kimaendeleo katika kata mbali mbali
za jimbo hilo pamoja na kuwasaidia madiwani wote 15 wa chama
cha mapinduzi (CCM) Power Tila vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya Tsh milioni 100.44
Lukuvi
alisema amelazimika kukabidhi msaada huo wa power tila kwa madiwani
wake ili kuwawezesha kiuchumi pia kusaidia kusukuma maendeleo
katika kata zao kama kuwasaidia wananchi kutumia power tila hizo
kuendeshea shughuli mbali mbali za kijamii zikiwemo za kilimo.
Kwani
alisema kuwa power Tila hizo amezinunua zikiwa na kamili ya vifaa
vyake vyote kama jembe la kulimia pamoja na tela zake kwa ajili ya
kusafirishia mazao ama kufanyia shughuli nyingine za kijamii katika
kata .
Akikabidhi
msaada huo leo kwa niaba ya mbunge Lukuvi katibu wake Thom
Malenga alisema kuwa kuwa lengo la msaada huo ni kusukuma mbele
maendeleo ya wananchi wa jimbo la Isimani na kuwa msaada wa bati
unakwenda katika kata zote ambazo zina miradi ya ujenzi wa shule
,nyumba za walimu na zahanati ambazo zilikuwa zikihitaji bati ili
kumalizia ujenzi huo na kuwa bati zote ziliotolewa ni 2000 zenye
thamani ya Tsh milioni 44
Wakati
msaada huo wa power Tila umeelekezwa kwa madiwani 15 wa CCM waliopo
katika jimbo hilo na kuwa kila power tila moja imegharimu kiasi cha
Tsh milioni 7 na kwa powertila zote zimegharimu Tsh milioni 105
lengo kubwa la kutoa msaada huo ni kuwawezesha madiwani hao kuwa na
vitega uchumi na kuongeza ari ya kuwatumikia wananchi wao .
Hivyo
alisema kuwa kupitia msaada huo wa bati anaamini madiwani hao
wakiwa ni wenyeviti wa kamati za maendeleo ya kata kuhakikisha
wanasimamia vema miradi ya ujenzi inayoendelea katika maeneo yao na
kwa upande wake mbunge ameamua kutoa msaada huo wa bati kama njia ya
kuwapunguzia makali wananchi wake kwa ajili ya kuchangia pesa kununua
bati hizo.
"
Mheshimiwa mbunge amewaunga mkono wananchi kwa kazi waliyoifanya
ya kusimamisha kuta za vyumba vya madarasa na zahanati na kwa ajili
ya kuwaunga mkono bati amelazimika kununua "
Hata
hivyo alisema kwa upande wa power Tila hizo alisema ni mradi
binafsi wa madiwani wake kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wao hivyo
kazi ya diwani na kusimamia shughuli za kimaendeleo na pale
wananchi wanapohitaji msaada wa power tila hizo basi mwenye mamlaka
nazo ni diwani mwenyewe na sio mradi wa kata wala kijiji .
Makamu
mwenyekiti wa Halmashauri ya Iringa na diwani wa kata ya Mboliboli
Khlfani Lulimi akishukuru kwa niaba ya madiwani wenzake alisema
kuwa msaada huo ni mkubwa kwao na zaidi wanampongeza mbunge wao kwa
kuthamini kazi inayofanywa na madiwani na kuwa watahakikisha power
tila hizo zinaleta chachu ya maendeleo katika maeneo yao.
Wakati
diwani wa kata ya Malenga Makali FLanzisca Kalinga na diwani wa viti
maalum tarafa ya Idodi Sophin Msekwa pamoja na kupongeza msaada huo
walisema wanategemea kutumia power tila hizo kwa ajili ya kuwasaidia
wanawake na watoto hasa ukizingatia kuwa kumwezesha mwanamke ni
kuisaidia jamii nzima.
|
Post a Comment