Header Ads

Serikali yasema Itaendelea Kushirikiana na Mashirika ya Kidini

Na Catherine Sungura, Muleba
Serikali inatambua na kuthamini mchango wa hospitali za mashirika ya dini katika kutatua matatizo ya wananchi nchini.

Hayo yamesema jana na waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu alipotembelea hospitali teule ya wilaya ya Rubya iliyopo wilayani Muleba

"Sera ya afya ni ileile hivyo tutaendelea kushirikiana katika kuboresha huduma zinazotolewa na madhebebu ya dini,hivyo bado ipo haja ya kufanya kazi nanyi"alisema

Waziri ummy alisema licha ya changamoto kubwa ya watumishi,wizara yake itaendelea kuwapangia watumishi katika hospitali hizo bila kudhoofisha utendaji wao

Alisema upungufu wa watumishi katika sekta ya afya nchini ni asilimia 48 ila kwa mkoa wa kagera upungufu ni asilimia 54,hivyo mkoa una uhaba mkubwa wa watumishi katika sekta ya afya.
Waziri wa afya Ummy Mwalimu akisalimiana na viongozi wa madhehebu ya kidini zinazomiliki  hospitali katika mkoa wa Kagera.
Aidha,amesisitiza hospitali hizo kufuata taratibu za kiutumishi kwa kutoa taarifa sahihi Za kuajiri mbadala wa watumishi wastaafu na wale wanaokufa ili kuondoa watumishi hewa na wale wasiokuwa na sifa kwa kulipwa malipo yasiyo halali.

"Hatutamlipa mtumishi mshahara kwa keshi kwa watumishi wote waliopo kwenye hospitali teule zinazomilikiwa na mashirika ya dini bali tunahitaji watumishi wote walipe kupitia akaunti zao za bank ili kuondoa tatizo lililopo hivi sasa

 Mkoa wa kagera ni miongoni mwa mikoa yenye hospitali nyingi zinazomilikiwa na mashirika ya dini nchini ambapo kati ya hospitali 14 za  mkoa huu,serikali ina miliki hospitali mbili tu.
Waziri Ummy Mwalimu akimjulia hali mama aliyejifungua katika wodi ya wazazi kwenye hospitali teule ya Rubyas.
Waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Ummy Mwalimu kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Mkoa wa Kagera,wilaya ya Muleba,Wamiliki wa hospitali teule ya Rubya pamoja na watumishi wa hospitali hiyo.

No comments

Powered by Blogger.