Header Ads

Serikali yakusudia Kuifanyia Marekebisho Sheria ya Ndoa

Serikali imedhamiria  kuifanyia marekebisho ya Sheria ya Ndoa na kuhakikisha marekebisho ya kifungu cha 13 na 17 cha sheria ya ndoa, kinachoruhusu mtoto chini ya miaka 18 kuolewa vinafanyiwa marekebisho kwa kuwasilisha muswada Bungeni kabla ya mwaka kuisha.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Mhe.Ummy Mwalimu wakati alipokua akiongea na ujumbe wa wanaharakati wa masuala ya maendeleo ya jinsia na watoto walipomtembele leo ofisini kwake

Waziri Ummy  alisema jitihada hizo za kufanya mabadiliko ya sheria zitahusisha pia sheria ya Mirathi inayomnyima mtoto wa kike na wanawake kurithi mali.
Ifuatie kabla ya  para ya mwisho.

Kuhusu uwakilishi wa wanawake katika vyombo vya maamuzi, mhe Ummy alisema bado ni suala la kipaumbele kwa Serikali na hasa kwa kuwa Tanzania imekubali Itifaki ya SADC ya Jinsia na Maendeleo ya Wanawake ya kufikia 50/50 ifikapo mwaka 2030.

Akizungumza kwa niaba ya ujumbe huo wa wanaharakati, mkurugenzi wa Mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP) bi. Liliani Liundi alisema  ipo haja ya Serikali kuongeza nguvu zaidi katika kuhakikisha sheria ya Ndoa kifungu cha 13 na 17 inafanyiwa marekebisho, kwakuwa inarudisha nyuma jitihada za kuleta usawa wa jinsia nchini.

Aidha, alieleza kuwa mabadiliko ya Sheria ya Elimu katika kifungu kinachokataza kuoa / kuoza mtoto wa shule ya Msingi na Sekondari ni jitihada inayohitaji kuungwa mkono.

“Ipo haja ya kuongeza nguvu zaidi katika kuwalinda watoto walio nje ya shule, kwakuwa mabadiliko haya ya sheria ya Elimu yaliyopitishwa na Bunge la 11 yawewaacha nje pasipo ulinzi wa sheria watoto wengi walio nje ya shule”Alisema.

Ujumbe wa wanaharakati uliwasilisha maoni yao na changamoto mbalimbali zinazo ikabili nchi katika kuleta maendeleo ya mtoto na usawa wa jinsia nchini, ikiwa ni pamoja na suala la Marekebisho ya Sheria ya Ndoa na Nafasi ya uwakilishi wa mwanamke katika vyombo mbalimbali vya maamuzi. Ujumbe huo uliongozwa na Mkurugenzi wa TGNP Mtandao Bibi Lilian Liundi na Wanaharakati wa Shirika la LHRC, WAJIKI, TANZANIA Widows Association na shirika la Wanawake katika Jitihada za Kimaendeleo (WAGIC)

No comments

Powered by Blogger.