Header Ads

Kuwait yaahidi Kuisaidia Tanzania Kwenye Sekta ya Afya


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Mhe.Ummy Mwalimu leo amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Jasem Al- Najem.

Katika mazungumzo yao Balozi Al-Najem ameahidi kuendeleza uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Kuwait.

Ikiwa ni katika kusaidia sekta ya Afya kwenye maeneo ya huduma ya Afya ya mama na mtoto, Upande wa upatikanaji  wa vifaa vya kujifungulia(Delivery Kits) vitakavyotolewa kwa wajawazito bila malipo, dawa na vifaa tiba pamoja na kutoa mafunzo kwa madaktari kwa kubadilishana wataalam kwa kipindi maalum.

Aidha Balozi huyo ameahidi kuisadia taasisi ya ya Moyo ya Jakaya Kikwete ili kuboresha utoaji wa huduma.


No comments

Powered by Blogger.