Dkt JOHN MAGUFULI, asema Nipeni Kura Zenu, Nikamilishe Ujenzi wa Barabara Zilizobaki !
mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli
akihutubia katika mkutano wa kampeni uliofanyika jioni ya leo kwenye
uwanja wa CCM wa Kigoda mjini Handeni na kuhudhuriwa na maelfu ya
wananchi wilayani humo, Dr Magufuli amewaomba wananchi wa Handeni
kumpigia kura za ndiyo ifikapo Oktoba 25 mwaka huu ili Rais na aweze
kuleta maendeleo na kakamilisha miradi mbalimbali ya barabara aliyoanza
kuitekeleza wilayani humo akiwa Waziri wa Ujenzi.
Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya
Wazazi ya CCM Ndugu Abdallah Bulembo ameitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi
na waangalizi wa kimataifa kutoa tamko kufuatia baadhi ya wagombea
kuanza kufanya kampeni chafu wakiingia makanisani na kujinadi na kuomba
kura makanisani jambo ambalo sio jema kwa taifa letu kwani siasa
haihusiani na masuala ya dini.
mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo wakati
akiwahutubia wananchi katika mkutano uliofanyika kwenye uwanja wa CCM
Kigoda mjini Handeni.
Umati wa wananchi ukifuatilia mkutano huo.
mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli akipanda jukwaani kwenye
mkutano uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Kigoda Handeni.
Baadhi ya wazee wa wilayani Kilindi wakiwa katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika kata ya Songe Kilindi.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Kilindi.
Kada wa CCM Ndugu Amon Mpanju akizungumza na wana Kilindi kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kijiji cha Songe.
Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Ndugu Abdallah Bulembo akiwahutubia wananchi katika mkutano huo.
Mzee Yusuf Makamba akiwahutubia wananchi wa kata ya Songe wilayani Kilindi wakati akimnadi Dr. John Pombe Magufuli.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli akizungumza na Mwenyekiti
wa CCM mkoa wa Tanga Hery Shekifu katikati nanyekiti wa Wazazi Ndugu
Abdallah Bulembo wananchi wa Kilindi.
Baadhi ya Akina mama wa wanachama wa CCM wakiimba huku wakiwa wameshika mabango yene picha ya Dr. John Pombe Magufuli.
Baadhi ya vijana wakimpungia
mkono Dr. John Pombe Magufuliwakati akiwa njiani kuelekea wilaya ya
Kilindi akitokea mkoani Morogoro.
Akina mama wakimpungia mkono Dr. John Pombe Magufuli.
Dr. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi njiani akitokea mkoani Morogoro kwenda Handeni Mkoani Tanga.
Hapa Kazi Tu!
Lazima tumuone Magufuli
Post a Comment