Header Ads

Dkt JOHN MAGUFULI, aahidi Kulinda Hali ya Usalama Kwa Watanzania Wote

 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akipanda ngazi kwa kukimbia kwenda jukwaani kujinadi kwa wananchi katika mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Taifa mjini Kibondo, Kigoma.

 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akijinadi kwa wananchi katika mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Taifa,  Kibondo, Kigoma

Akihutubia kwa nyakati tofauti, katika mikutano ya  kampeni zake mkoani Kigoma, amekuwa akihimiza kudumisha amani nchini ambapo pia aliwataka viongozi wa kisiasa  kuhubili sulala hilo katika mikutano yao.

PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akijinadi kwa wananchi katika mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Umoja  Kasulu, Kigoma.

 Wananchi wakimsikiliza kwa makini Dk ,Magufuli alipokuwa akijinadi katika Jimbo la Buhigwe, Kigoma.

 Dk Magufuli akihutubia alipokuwa akifanya kampeni  katika Kijiji cha Munanila, wilayani Buhigwe, Kigoma.

 Dk Magufuli akimnadi mgombea ubunge jimbo la Buhigwe Albert Ntabaliba 'Obama' huku mmoja wa wagombea udiwani askishangilia wakati wa mkutano wa kampeni mjini Munanla Buhigwe, Kigoma leo.

 Mkazi wa Mji wa Munanila akisikiliza kwa makini Dk Magufuli alipokuwa akijinadi kwa wananchi katijka Jimbo la Buhigwe.

 Wananchi wakishangilia hotuba ya Dk Magufuli huku wakiwa na matawi ya miti  katika Mji wa Munanila, Jimbo la GBuhigwe, Kigoma.

 Mama akiwa na mkungu wa ndizi alipokuwa akimsikiliza Dk Magufuli katika Kijiji cha Mvugwe wilayani Kasulu.

 Wananchi wakishangilia wakati Dk Magufuli akijinadi mjini Buhigwe, Kigoma leo.

 Dk Magufuli akimnadi mgombea ubunge jimbo la Buhigwe Albert Ntabaliba 'Obama' katika kkiutano wa kampeni katika mji wa Buhigwe.

 Ni furaha iliyoje kwa wananchi baada ya kufurahishwa na sera za CCM zilizokuwa ziktolewa na Dk Magufuli katika mkutano wa kampeni mjini Buhigwe leo.

  Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akijinadi kwa wananchi katika mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Umoja  Kasulu, Kigoma.

 Dk Magufuli akiwanadi Daniel Nsanzugwako (kulia) anayegombea ubunge kupitia CCM katika Jimbo la Kasulu Mjini na Agustino Zuma Ole anayewania ubunge jimbo la Kasulu Kusini kupitia chama hicho.

 Dk Magufuli akimkabidhi Mgombea ubunge Jimbo la  Kasulu Kusini, Agustino Ole Ilani ya Uchaguzi ya CCM wakati wa mkutano huo wa kampeni.

 Wananchi wakimrekodi kwa simu Dk Magufuli  alipokuwa akihutubia katika moja ya vijijini wilayani Kibondo leo.

 Akina mama na watoto wakigombea picha za Dk Magufuli mjini Kibondo wakati wa mkutano wa kampeni.

 Mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya CCM, Abdallah Bulembo alkielezea wasifu wa Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk Magufuli katika mkutano wa kampeni mjini Kibondo.

 Sehemu ya umati wa wananchi katika mkutano wa kampeni za CCM MJINI Kibondo.

 Dk Magufuli akimkabidhi Mgombea ubunge Jimbo la Muhambwe kupitia , Injinia Atashasta Nditie Ilani ya Uchaguzi ya chama hicho.

Mratibu wa Magufuli kwa Maslahi kwa Umma Mkoa wa Kigoma, Silvia Sigula (kushoto) na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Mkoa wa Kigoma Peter Msangula wakishangilia baada ya kupendezewa na hotuba ya Dk Magufuli katika mkutano wa kampeni mjini Kibondo leo.

No comments

Powered by Blogger.