Header Ads

Maalim SEIF SHARIF HAMAD, akutana na Balozi wa Qatar, Sheikh ABDULLA JASSIM AL-MAADADI

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na balozi wa Qatar nchini Tanzania Sheikh Abdulla Jassim Al-Maadadi, nyumbani kwake Mbweni.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akimsindikiza balozi wa Qatar nchini Tanzania Sheikh Abdulla Jassim Al-Maadadi, baada ya mazungumzo yao nyumbani kwake Mbweni.
 ........................................................................
 
Qatar imesema inakusudia kuendeleza uhusiano wa kindugu uliopo kati yake na Zanzibar, sambamba na kukukuza mahusiano ya biashara na uchumi.
 
Balozi wa Qatar nchini Tanzania Sheikh Abdulla Jassim Al-Maadadi ameeleza hayo leo alipokuwa na mazungumzo na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, nyumbani kwake Mbweni.
 
Amesema Qatar na Zanzibar zina uhusiano wa muda mrefu ambao unapwa kuendelezwa katika nyanja zote za maisha kwa maslahi ya pande zote mbili.
Balozi Al-Maadadi ameelezea kuridhishwa na mazingira ya Zanzibar na kuahidi kushirikiana na Jumuiya ya wawekezaji ya Qatar, ili kuangalia uwezekano wa kuwekeza miradi yao ya kiuchumi.
 
Amesema Zanzibar ni pahala pazuri pa kuwekeza, hivyo atafanya juhudi kuona kuwa wawekezaji wa Qatar wanaelekeza nguvu za kuwekeza visiwani Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.
 
Nae Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amumuhakikishia balozi huyo kuwa Zanzibar ni mahala salama kwa uwekezaji.
Amesema mbali na mazingira mazuri yaliyopo, ukarimu na utamaduni wa Wazanzibari ambao unalingana na ule wa watu wa Qatar, unachukua nafasi kubwa kuweka mazingira bora ya uwekezaji kwa wawekezaji wa Qatar.
 
Amesema Zanzibar na Qatar zinaweza kushirikiana katika maeneo mbali mbali yakiwemo uvuvi wa bahari kuu pamoja na utalii, huku akishajiisha utalii wa daraja la juu.
 
Maalim Seif ameelezea matumaini yake kwa wafanyabiashara na wawekezaji wa Qatar kuja kuwekeza Zanzibar, ambapo pia amezungumzia ziara yake aliyoifanya nchini Qatar hivi karibuni na kukutana na viongozi wakuu pamoja na Jumuiya ya wafanyabiashara wa nchi hiyo.
 
Aidha Maalim Seif ametoa wito kwa kampuni za uchimbaji wa mafuta na gesi za nchini Qatar kukaa tayari, kwani Zanzibar inajiandaa kutoa tenda za uchimbaji wa mafuta na gesi katika siku za hivi karibuni.
 
Katika hatua nyengine, Maalim Seif amesema serikali inakusudia kuuimarisha uwanja wa ndege wa Pemba, ili kukifungua kisiwa cha Pemba kibiashara na utalii.
Makamu huyo wa Kwanza wa Rais amesema kisiwa cha Pemba kimekuwa na utajiri mkubwa katika sekta ya kilimo hasa zao la Karafuu ambalo ni tegemeo kubwa kwa wakulima wa zao hilo na Taifa kwa ujumla, na kutoa wito wa kuendelezwa.
 
Sambamba na hilo Maalim Seif amewataka wananchi kukiendeleza kilimo cha minazi, ili kuliendeleza zao hilo la kihistoria visiwani Zanzibar kuweza kusaidiana na zao la karafuu kwa lengo la kukuza uchumi na kipato cha wananchi.
 

No comments

Powered by Blogger.