Header Ads

Mgombea Urais wa Chadema, EDWARD LOWASSA, azungumza na Wananchi wa GAIRO na KIBAIGWA

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiteta jambo na Mwanasheria wa CHADEMA, Mh. Tundu Lissu, wakati wa Mkutano wa Kampeni za Mgombea huyo, uliofanyika kwenye Uwanja wa Amani, Kibaigwa Mkoani Dodoma leo Septemba 10, 2015. 

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Jimbo la Gairo Mkoani Morogoro, wakati wa Mkutano wa Kampeni unaoambatana na kunadi sera za chama chake, uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Gairo Mkoani Morogoro, leo Septemba 10, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akimsikiliza Mgombea Ubunge wa Ukawa kupitia CHADEMA wa Jimbo la Gairo, Salum Mpanda, wakati akimuelezea changamoto zinazowakabili wananchi wa Jimbo hilo, katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Gairo Mkoani Morogoro, leo Septemba 10, 2015. Kulia ni Waziri Mkuu mstaafu, Mh. Fredrick Sumaye.
Waziri Mkuu mstaafu, Mh. Fredrick Sumaye, akiwaonyesha wananchi wa Jimbo la Gairo, Mkoani Morogoro, Kiberiti chenye picha ya Mgobea Ubunge wa CCM wa Jimbo hilo, na kuwataka wasirubunike kirahisi kwa kupewa kitu cha namna hiyo, wakati wa Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Gairo Mkoani Morogoro, leo Septemba 10, 2015. 
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwanadi baadi ya Wagombea UKAWA wa nafasi ya Udiwani kutoka Kata mbali mbali za Jimbo la Gairo, Mkoani Morogogo leo Septemba 10, 2015. Picha na Othman Michuzi.


No comments

Powered by Blogger.