Wilaya za Mkuranga, Rufiji na Kibiti Kuunganishwa Umeme wa Gridi ya Taifa
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard
Kalemani amesema Wilaya za Mkuranga, Rufiji pamoja na Kibiti mkoani Pwani zitaunganishwa
katika Gridi ya Taifa wakati wa kuanza kwa Awamu ya Tatu ya utekelezaji wa
Mradi Umeme Vijijini unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa
kushirikiana na Shirika la Umeme Tanzania ( TANESCO).
Dkt. Kalemani alisema hayo wakati wa ziara yake ya
siku moja ya kukagua maendeleo na utekelezaji Mradi wa Umeme Vijiji katika Wilaya hizo pamoja na kuzungumza na wananchi.
Alifafanua kuwa ni lazima Wilaya hizo
zikaungwanishwa katika Gridi ya Taifa ili waweze kupata umeme mwingi, wa
kutosha na wa uhakika ili kuongeza kasi na ufanisi katika shughuli za wananchi
za kujipatia maendeleo.
dkt. kalemani aliweka wazi kuwa wakati wa
kutekeleza awamu ya tatu ya mradi wa rea, tanesco itajenga kituo kikubwa cha
kupokea na kupoza umeme katika Wilaya ya
Mkuranga ili kusambaza katika Wilaya hizo.
Post a Comment