Mkurugenzi Msaidizi
Ufuatiliaji na Tathmini (Sekta ya Uchukuzi), Bw. Aunyisa Meena akifafanua jambo
katika kikao kazi kujadili namna ya kushirikiana katika ujenzi wa miundombinu
ya kisasa baina ya viongozi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na
wadau wa maendeleo, Jijini Dar es salaam.
Profesa Mbarawa
amesisitiza kwamba Serikali imejipanga kudhibiti rushwa ili fedha nyingi
zinazotumika katika miundombinu ilete matokeo chanya na kuwahakikishia kwamba
ujenzi wa reli ya kisasa ya kati (Standard Gauge), itaanza baadaye mwaka huu na
ikikamilika itapunguza gharama kubwa za usafirishaji zinazotumika kupitia
malori.
Profesa Mbarawa
amewashukuru wadau wa maendeleo kwa misaada mbalimbali wanayotoa katika sekta
ya ujenzi wa barabara na ukarabati wa reli mara kwa mara na kusisitiza kwamba Serikali
inatambua na kuthamini michango hiyo na kuomba washirikiane katika ujenzi wa reli
ya kisasa ya kati (Standard gauge).
Zaidi
ya kilomita 2600 za Reli ya Kisasa (Standard gauge) zinatarajiwa kujengwa
kutoka Dar es Salaam-Morogoro-Dodoma-Tabora-Isaka hadi Mwanza ambayo ni uti wa
mgongo wa reli hiyo.
Na
Sehemu nyingine ni kutoka Tabora-Mpanda hadi Kalemela na Tabora-Uvinza hadi
Kigoma ambayo itaunganisha na nchi za Rwanda na Burundi na hivyo kufungua
huduma za kiuchumi na uchukuzi kati ya Tanzania na nchi za maziwa makuu.
|
Post a Comment