Maporomoko Lusingizo yenye mita zaidi ya 50
yaliyoko katika Hifadhi ya Mazingira Asili ya Mkingu ambayo ni mojawapo ya kivutio cha Utalii
katika Hifadhi hiyo, Hadi hivi sasa kuna
wawekezaji wamejitokeza ili waweze kuzalisha umeme katika kivutio hicho cha
utalii.
Mbali ya
kupatikana kwa wanyama na mimea katika Hifadhi hiyo Bw, Kindo anaeleza kuwa kuna
pango la Malolo ambalo wenyeji wa Mkindo
wana historia kubwa ya pango hilo ambalo wenyeji hawataweza kusahau kwani kuna mwanaume
mmoja aliiba mke wa Mtu akaishi naye
ndani ya pango hilo kwa muda wa miaka 3 bila kujulikana kijini. Pango hilo lina vyumba mithili
ya nyumba iliyojengwa.
Pia anasema kuwa nadni ya hifadhi hiyo kuna pango ambalo ukikaa nje kuna upepo
unaotoka ndani unapuliza hiyo ni ishara tosha kuwa humo ndani ndani kuna uhai.
Anabainisha kuwa hifadhi hiyo ina jiwe lenye alama za nyayo za binadamu, kwato
za mifugo ikiwa hiyo ni ishara tosha
kuwa maisha ya kale ya binadamu
yalianzia ndani ya hifadhi hiyo.
Aliongeza kuwa mbali ya mapango ndani ya hifadhi hiyo , kuna maporomoko
Lusingizo yenye mita zaidi ya 50 , hadi
hivi sasa kuna wawekezaji wamejitokeza ili waweze kuzalisha umeme katika kivuto
hicho cha utalii.
Pia kuna magofu ya kale ya Wajerumani ambayo waliishi
ndani ya hifadhi kabla vita vya pili vya dunia na baada ya kuondoka kwa
Wajerumani ilikuwa shule ya msingi
ya kijiji cha Mafuta, na baada ya eneo hilo likatangazwa kuwa
hifadhi , Shule ile ilitolewa na
kujengwa kijijini.
Bw. Kindo anasema licha ya hifadhi hiyo kuwa na
vivutio lukuki bado imekuwa ikitembelewa
na idadi ya watalii isiyoridhisha licha kwa mwaka
jana wameweza kupata watalii 75 kutoka Ujerumani.
‘’Tokea mwaka jana hadi hivi sasa tumeweza kuibua
vivutio saba vya utalii na tunaendelea kufanya jitihada za makusudi ili kuhakikisha tunakuwa na vivutio vingi vya
utalii ili tuweze kuwavutia watalii wa ndani na nje ya nchi ‘’.alisema Bw.
Kindo.
Aidha,Alisema Hifadhi hiyo ndio chanzo cha mto Wami, mto Ruvu na Mto Mkingu ambapo maji hayo yamekuwa
yakitumika katika shughuli za kiuchumi kama vile kilimo,uvuvi,mazalia na makazi
ya mimea na wanyama bila kusahau maji hayo ndiyo hutumika kuwanyesha wakazi wa
Dare s Salaam na mikoa ya jirani.
Amewataka wanafunzi wa vyuo mbalimbali wasisubili watafiti kutoka nje ya nchi kwenda
kufanya tafiti katika Hifadhi hiyo badala yake wao wawe mstari wa mbele katika
kuvumbua vitu vingi ambavyo vinapatikana katika hifadhi hiyo
|
Post a Comment