Header Ads

UVCCM kufanya Maandamano ya Amani Agosti 31 Kumpongeza Rais Dkt MAGUFULI

Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Shaka Hamdu Shaka akiwaonesha Waandishi wa habari barua walioiandikia Jeshi la Polisi kuomba kibali na Ulinzi cha kufanya Maandamano hayo ya amani,wanayotarajia kufanya Agosti 31,kwa minajili ya kumpongeza na kueleza Wananchi utendaji kazi wa Rais Dkt John Pombe Magufuli.

OTH_8200
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Shaka Hamdu Shaka akitoa ufafanuzi kwa baadho ya maswali mbalimbali yaliyokuwa yakiulizwa na Waandishi wa habari kuhusiana na Maandamano hayo ya amani yanayotarajiwa kufanyika Agosti 31,kwa minajili ya kumpongeza na kueleza Wananchi utendaji kazi wa Rais Dkt John Pombe Magufuli.

Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Shaka Hamdu Shaka akizungumza na Waandishi wa habari Makao makuu ya Ofisi hizo mapema leo jijini Dar kuhusiana na kufanya maandamano ya amani Agosti 31,kwa minajili ya kumpongeza na kueleza Wananchi utendaji kazi wa Rais Dkt John Pombe Magufuli.

 
Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) wanatarajia kufanya maandamano ya Amani Agosti 31 kwa ajili ya kueleza utendaji kazi wa Rais Dk.John Pombe Magufuli kwa Watanzania.
 
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja huo, Shaka Hamdu Shaka amesema kuwa maandamano hayo wameshamwandikia barua mkuu wa jeshi la Polisi kwa ajili ya kupata ulinzi siku hiyo’
 
Amesema kuwa wasipopata ulinzi watafanya kwa kujilinda wenyewe ikiwa ni lengo la kufikisha ujumbe kwa wananchi juu ya utendaji kazi wa Rais Dk. John Pombe Magufuli.Shaka amesema kuwa Rais Dk.John Pombe Magufuli amefanya watendaji kuwa na utii pamoja na maadili katika utoaji wa huduma kwa wananchi.
 
Aidha amesema kuwa maandamano hayo wanaawalika na vijana wa vyama vingine kushiriki kwa lengo moja tuu,la kuunga mkono utendaji wa Rais Dkt.John Pombe Magufuli.
 
Shaka ameongeza kuwa hawana nia mbaya katika maandamano, “kiu yetu kutaka kufikisha ujumbe kwa wananchi juu ya Rais anachokifanya katika kuwaletea huduma na Maendeleo Watanzania”,alisema Shaka.

No comments

Powered by Blogger.