Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Huduma za Misitu Tanzania ( TFS) imepiga marufuku usafirishaji wa mazao ya
misitu ikiwemo mkaa ambapo mfanyabiashara anayefanya biashara hiyo, atapaswa
kuwa na vigezo ambavyo Serikali inavihitaji, tofauti na hapo sheria itachukua
mkondo wake.
Imesema zuio hilo linakwenda sambamba na kupiga marufuku usafirishaji wa magogo
ya miti kwenda nje ya nchi, magari kubeba mbao yakiwa yamefunikwa, pikipiki na
baiskeli kubeba mkaa kwenda sehemu moja hadi nyingine mijini na
vijijini.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mtendaji Mkuu wa
Wakala wa Misitu Tanzania (TFS), Profesa Dos Santos Silayo, alisema uamuzi huo
ni moja ya mikakati ya kukusanya maduhuli stahiki ya rasilimali za misitu na
kuwabana wakwepa ushuru.
|
1. Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Prof. Dos Santos Silayo akizungumza
na Waandishi wa habari leo, Mpingo House jijini Dare Salaam, kuhusiana na
utaratibu wa kusafirisha mazao ya misitu ikiwemo mkaa ambapo
mfanyabiashara anayefanya biashara hiyo, atapaswa kuwa na vigezo ambavyo
Serikali inavihitaji, tofauti na hapo sheria itachukua mkondo wake.
Alisema moja ya majukumu ya TFS, ni kuhakikisha inaanzisha na kusimamia
rasilimali za misitu ili zisaidie ustawi wa taifa kwa kizazi cha sasa na
kijacho, hivyo ni lazima wananchi wafahamu kuwa ni kosa kuvuna hovyo misitu na
bidhaa zake bila kibali.
Mtendaji huyo alisema kila zao
linalotokana na misitu ni lazima lilipiwe ushuru stahiki na kukatiwa risiti,
hivyo kukwepa kufanya hivyo kwa kutumia njia mbalimbali zinazokatazwa ni kuvunja
sheria na kuiibia serikali mapato.
"Mazao ya misitu, ikiwemo mikaa ni kosa kuuzwa na kusafirishwa bila kuwepo
kibali na risiti. Muuza mkaa lazima uwe na risiti, na wewe mnunuzi tukikukamata
na gunia la mkaa na huna risiti utawajibika.
"Tunataka kuhakikisha maduhuli ya mazao ya misitu yanakusanywa ili kupata
matumizi endelevu ya rasilimali za misitu hivyo ni biashara hii ya miti, mkaa
na mazao ya nyuki inatakiwa iwe wazi.
|
|
1. Mkurugenzi wa
Mipango na Matumizi Endelevu ya Rasilimali za Misitu wa Wakala wa Huduma za
Misitu Tanzania (TFS) Bw. Mohammed Kilongo akitoa
ufafanuzi leo, Mpingo House jijini Dare Salaam, kuhusu upigaji marufuku
usafirishaji wa magogo ya miti kwenda nje ya nchi, magari kubeba mbao yakiwa
yamefunikwa, pikipiki na baiskeli kubeba mkaa kwenda sehemu moja hadi nyingine
mijini na vijijini. Kulia ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa
Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Prof. Dos Santos Silayo.
"Ni marufuku kusafirisha mazao ya misitu usiku, kama mtu ana vigezo
vyote tunavyovihitaji kusafirisha mazao ya misitu anatakiwa kusafiri kuanzia
saa 12 asubuhi mpaka saa 12 jioni, ikipita hapo, weka pembeni gari mpaka
asubuhi," alisema.
Aidha alisema TFS chini ya Wizara ya Maliasili ina Meneja miti kwenye kila
wilaya, ambao wanafanya kazi kwa karibu na Maofisa Watendaji wa vijiji ambao
hushirikiana kutoa vibali kwa kuvuna miti stahiki kisheria na kutoa risiti.
Alisema risiti hizo pamoja na vigezo vingine ikiwemo kuwa na usajili wa TFS,
leseni ya biashara na namba ya utambulisho wa mfanyabiashara (TIN), hati ya
kusafirisha mazao ya misitu humfanya mfanyabiashara kuruhusiwa kuendelea na
biashara ya mazao ya miti nchini.
|
|
1. Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Prof. Dos Santos Silayo
(kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa
Mipango na Matumizi Endelevu ya Rasilimali za Misitu wa Wakala wa Huduma za
Misitu Tanzania (TFS) Bw. Mohammed Kilongo (Kulia) wakizungumza na Waandishi wa
habari leo, Mpingo House jijini Dare
Salaam, kuhusiana na utaratibu kusafirisha
mazao ya misitu ikiwemo mkaa ambapo mfanyabiashara anayefanya biashara
hiyo, atapaswa kuwa na vigezo ambavyo Serikali inavihitaji, tofauti na hapo
sheria itachukua mkondo wake.
Profesa Silayo alisema
TFS wataendelea na majukumu yao kwa ufanisi ikiwa ni pamoja na kutekeleza
maagizo yaliyotolewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, alipozungumza na
watumishi wa wizara hiyo mapema mwezi uliopita.
Baadhi ya maagizo hayo likiwemo la kupunguza vizuio kwenye maeneo mbalimbali ya
nchi, Silayo alisema wanafanya utafiti kujua kizuizi gani kitolewe na kipi
kibaki sambamba na kubana uvunaji holela wa misitu.
Alisema lengo lao si kukamata magogo baada ya kuvunwa bali ni kuzuia misitu
isiharibiwe hivyo inapotokea, hutumia vizuio hivyo kukagua na kukamata nyara
hizo za serikali ili kuongeza maduhuli kwa mujibu wa sheria.
"Tumeanza kutekeleza maagizo ya Waziri Mkuu, ambayo kiuhalisia yana ukweli
mkubwa kwa hiyo tunataka kuondoa vizuizi visivyo na tija lakini pia
kuwasisitizia watu wetu kule vituoni kuzingatia weledi.
"Tayari tumeanza kutumia mashine za kielektroniki za malipo yaani EFD
kwenye vizuio vyetu mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Morogoro na tutaendelea
kuzisambaza maeneo mengine mara tu TRA watakapoziingizia program yao ya
malipo," alisema.
Alisema wana changamoto kadhaa ikiwemo uhaba wa vitendea kazi hususan magari
lakini wanafanya jitihada mbalimbali kuhakjikisha wanazitatua ili misitu iwe na
mchango kwenye pato la taifa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mipango na Matumizi Endelevu ya Rasilimali Misitu
wa TFS, Mohammed Kilongo, alisema
kitakwimu asilimia 94 za kaya zote takriban milioni tisa nchini zinatumia mkaa
kama nishani kuu, huku maeneo ya mijini pekee ikiwa na asilimia 38 za watumia
mkaa.
"Mahitaji ya miti ni mita za ujazo 62.3 huku uwezo ukiwa ni mita za ujazo
42.8 hivyo uharibifu wa misitu unafika hekta 372,000 kwa mwaka sawa na asilimia
1.1 ya eneo lote lenye miti," alisema Kilongo.
Alisema kwa takwimu hizo, miti na misitu nchini imekuwa ikipungua kwa kiasi
kikubwa na kusababisha uhitaji wa hekta mpya 185,000 za misitu inayotakiwa kupandwa
maeneo mbalimbali ya nchi.
"Upungufu huu ni kichocheo cha uvunaji haramu na holela ndani ya misitu ya
hifadhi, mapori ya akiba na hata ndani ya hifadhi za taifa hivyo suala la
kuilinda ni jukumu letu sote, kila gunia lazima lilipiwe ushuru," alisema.
Pia alisema katika jitihada za kurudisha misitu iliyopotea, upo mkakati wa
kitaifa wa kupanda miti ambapo kwa kila wilaya imepewa jukumu la kupanda miti
milioni moja na nusu kwa mwaka chini ya uangalizi wa Meneja misitu wa wilaya
husika.
Wiki kadhaa zilizopita, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa
Wizara ya Maliasili na Utalii jijini Dar es Salaam, alisema nchi inageuka
jangwa kutokana na misitu mingi kukatwa kiholela huku maduhuli ya serikali
yakipotea.
Kauli hiyo inaonekana kuanza kuzaa matunda baada ya TFS kuamua kuongeza kasi ya
usimamizi wa rasilimali za misitu na nyuki nchini kwa siku za hivi karibuni
hatua ambayo inadaiwa kuwa endelevu.
TFS inasimamia jumla ya misitu 506 nchini ikiwemo ya asili na kupandwa, pamoja
na kusimamia jamii takriban milioni 9.2 za nyuki walioko kwenye misitu hiyo
maeneo mbalimbali ya nchi.
|
Post a Comment