Serikali yakitoza Faini ya Shilingi Milioni Kumi Kiwanda cha MO ENTERPRISES
Kiwanda cha kutengeneza maji na juice cha cha MO ENTERPRISES kimetozwa faini ya
shilingi milioni kumi kwa kosa la kumwaga maji machafu katika makazi ya watu,
bila kupata kibali cha Baraza la taifa la Usimamizi wa Mazingira NEMC na kibali
cha Bonde la wami ruvu, kinachoruhusu kuachia maji yaliyotibiwa kwenye
mazingira.
Hayo yamebainika katika muendelezo wa oparesheni ya ukaguzi wa
mazingira na viwanda jijini Dar Es Salaam
inayofanywa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.
Luhaga Mpina.
Kiwanda hicho kinatakiwa kulipa faini ya shilingi milioni
kumi kwa muda wa siku saba, pamoja na kufanya marekebisho ya miundominu
kiwandani hapo na kupata kibali cha kutiririsha maji wanayoyatibu toka
kiwandani hapo, kutoka kwa Baraza la Taifa la Hifadhi na usimamizi wa Mazingira
NEMC.
Katika ziara Hiyo, NEMC pia imewatoza faini ya shilingi milioni
tano kila moja wakazi tisa wa eneo la kiwalani Bam Bam kwa kile kinachodaiwa ni
kutapisha maji ya vyoo katika mfereji mkubwa wa maji ya mvua maarufu kwa jina
la mfereji wa Airport, Nakutakiwa
kulipa faini hiyo ya jumla ya shilingi milioni arobaini na tano kwa muda wa
wiki moja , kinyume na hapo watafikishwa mahakamani.
Aidha, Naibu Waziri Mpina pia alitembelea kiwanda cha Step Entertainment kinachotengengeza CD, tape na DVD na kujionea
uchafuzi wa mazingira kwa kutiririsha maji ya chooni katika mazingira na
kuwatoza faini ya shilingi milioni saba ambayo inatakiwa kulipwa ndani ya siku
saba pamoja na kuwataka kuziba matoleo yote ya mifereji inayotoa maji machafu
na kufanya usafi wa mazingira mara moja.
Timu hiyo ya Naibu Waziri Mpina pia ilitembelea kiwanda cha Royal na kukipa AMRI kali la kufanya kusafi wa mazingira katika mtaro wao kwa muda
wa siku mbili.
Post a Comment