Mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdulah ametangaza kuwachukulia hatua kali wananchi watakaopuuza agizo la Rais Dr John Magufuli na kufanya usafi wa mazingira yanayowazunguka kila juma la mwisho la mwezi .
Huku akipiga marufuku kilimo cha mahindi nje ya ofisi yake kuwa kuendelea kulima mahindi na mazao yanayozidi futi tatu katika eneo linalozunguka ofisi yake ni moja ya uchafuzi wa mazingira na kuwa kuanzia sasa mazao marefu katika maeneo yote yanayozunguka ofisi za umma ni marufuku .
Mkuu huyo wa wilaya alitoa kauli hiyo juzi baada ya kuongoza oparesheni ya usafi kwa watumishi wa Halmashauri ya Kilolo na wanafunzi wa shule ya sekondari Kilolo kufanya usafi maeneo ya jengo la ofisi ya mkuu wa wilaya ya kilolo jengo ambalo nyoka walikuwa wakitishia usalama wa watumishi wa ofisi hiyo kutokana na jengo hilo kuzungukwa na nyasi ndefu na vichaka kwa zaidi ya miaka 10 .
Akizungumza baada ya zoezi hilo mkuu huyo wa wilaya aliwapongeza wakuu wa idara katika halmashauri ya Kilolo pamoja na wananchi ambao waliitikia wito wa kufanya usafi huku akisema idadi ya wananchi waliofika kufanya usafi hajafurahishwa nao kwani ni wananchi wachache ambao walitoka kufanya usafi pamoja na gari ya matangazo kupita mitaani kabla ya siku ya usafi na kuhamasisha wananchi kushiriki zoezi hilo .
|
Post a Comment