Wakati chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Nyanda za Juu
Kusini (Nyasa) kikitangaza kikijiandaa kwa utekelezaji wa azimio ya kamati kuu cha Chadema chini ya mwenyekiti wake Taifa Bw
Freeman Mbowe kwa kujipanga kwa oparesheni UKUTA
,mkuu wa mkoa wa Iringa Bi Amina Masenza (pichani)amepiga marufuku
maandamano ya vyama vya siasa wala viongozi wageni kutoka nje ya
mkoa wa Iringa kufanya mikutano ndani ya mkoa huo.
Mkuu
huyo wa mkoa aliyasema hayo jana wakati akizungumza na wanahabari
ofisini kwake kuhusiana na utekelezaji wa ilani ya CCM na utekelezaji
wa agizo la Rais Dr John Magufuli la kuzuia maandamano na mikutano ya
kichochezi nchini.
"
Mikutano inayoruhusiwa ni ile ya madiwani na wabunge katika
majimbo yao .....hivyo naomba kuelekewa sitakubali kuona maandamano
wala viongozi wa vyama vya kisiasa kutoka nje ya majimbo ama kata
husika kuja kufanya mikutano ama maandamano katika jimbo ama kata
nyingine"
Mkuu
huyo wa mkoa alisema kuwa hakuna diwani wala mbunge ambaye
amezuiliwa kufanya mikutano ya kimaendele katika eneo lake na kuwa
mikutano inayozuiwa ni ile ya vyama vya siasa ambayo kimsingi muda
wake bado haujafika na pindi muda wa siasa ukifika vyama vitaruhusiwa
kufanya siasa ila kwa sasa ni wakati wa kufanya kazi za kuwaletea
wananchi maendeleo.
"
Kila jambo linawakati wake suala la siasa lilimalizika baada ya
uchaguzi mkuu na tayari madiwani ,wabunge na Rais amekwisha
patikana kinachoendelea sasa ni wale waliochaguliwa kuwatumikia
wananchi kwa kufanya kazi si vinginevyo "alisisitiza mkuu huyo wa
mkoa
kuwa
katika kata zote na majimbo yote ya mkoa wa Iringa angependa
kuona wanaofanya mikutano ya kimaendeleo ni wahusika wa maeneo hayo
na sio watu kutoka nje ya maeneo husika .
Katika
hatua nyingine mkuu huyo wa mkoa wa Iringa alisema kuwa hata
madiwani na wabunge ambao wameruhusiwa kufanya mikutano ya
kimaendeleo katika maeneo yao ,serikali ya mkoa huo haitawavumilia
wale wote watakaotumia vibaya nafasi hiyo kwa kutukana amakumsema
vibaya Rais ama chama kingine cha siasa.
“Kwa ujumla wake (Mkoa wa Mbeya, Songwe, Rukwa, Iringa na
Njombe) inaunga mkono maazimio ya Kamati kuu ya Chama Chetu iliyoketi tarehe
27/07/2016 ya kupinga vikali aina zote za udikteta zinazoendelea na kufanywa na
serikali ya chama cha Mapinduzi (CCM)….. na kuwa tupo tayari kuona Demokrasia
ya vyama vingi nchini Tanzania inaendelea kuimarika kama iliyo asisiwa na Baba wa Taifa Mwal. Julius kamabarage
Nyerere, ambayo aliiacha ikiwa na amani na utulivu na kuwa nchi yenye kuruhusu
mfumo wa vyama vingi”
Mwaisumbi alisema
utakuwa ni uonevu mkubwa
iwapo serikali ya CCM itazuia
Chadema kuendelea na
Oparesheni UKUTA wakati juzi Dodoma katika Uwanja
wa Jamhuri aliyekuwa mwenyekiti
wa CCM Taifa Rais Mstaafu
Dr Jakaya Kikwete
alifanya mkutano mkubwa
ambao kimsingi si mkutano wa kiserikali ila ulikuwa ni mkutano wa Chama.
Bw Mwaisumbialisema
wao kama Chadema kanda ya Nyasa watahakikisha wanafanya
zoezi hilo la Oparesheni UKUTA
pasipo kuvuruga amani ya
nchi na kuona mikutano yao
yote inafanyika kwa uhuru na
amani na wapo tayari
kuendelea kulinda amani na
utulivu.
“ sisi CHADEMA kanda ya Nyasa kwa pamoja tunajiunga na UKUTA Umoja
wa Kupinga Udikteta Tanzania.. wa UKAWA na tupo tayari wakati wote kupambana na
mtu yeyote anayevunja katiba na kuweka udikteta…. hii ni nchi yetu sote na
tupewe uhuru kwa usawa bila kuvunja katiba ya nchi”
Wakati
huo huo mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa
katika mkutano wake wa hadhara alioufanya siku moja kabla ya mkuu wa
mkoa wa Iringa kupiga marufuku maandamano na mikutano ya wanasiasa
toka nje ya kata na majimbo husika ,alisema kinachofanywa na serikali
kupiga marufuku mikutano ya vyama ni kuua Demokrasia nchini na kuwa
suala hili halitavumilika.
Mchungaji
Msigwa alisema kuwa pamoja na kuwa mkutano wake huo ulikuwa wa
jimbo kwa ajili ya maendeleo ila pindi chama chake kitakapo agiza
kuanza kwa oparesheni UKUTA atawajulisha wapiga kura wake.
Post a Comment