Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Meneja wa
Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Mkoa wa Rukwa Arch. Deocles Alphonce wakati
alipokagua ujenzi wa ofisi za Bonde la Ziwa Rukwa na Maabara zake zilizopo
Sumbawanga Mjini.
“Nataka
TPA muanze kutumia video Conference katika vikao vyenu ili fedha zilizokuwa
zikitumika zifanyie kazi nyingine za maendeleo ya Taifa”, amesema Waziri Prof.
Mbarawa.
Ameongeza
kuwa TPA imekuwa na wajibu mkubwa wa
kuchangia pato la Taifa kupitia huduma za upakiaji na upakuaji wa mizigo hivyo
wanapaswa kuanza kutumia mfumo wa kielekroniki katika ukusanyaji wa mapato
katika bandari zote nchini ili kudhibiti upotevu wa mapato.
“Tukianzisha
mfumo wa kielekroniki katika bandari hii tutakuwa na uwezo wa kufuatilia mapato
yanayopatikana katika utoaji wa huduma na kujua kama malengo yamefikiwa”,
amesema Prof. Mbarawa.
|
Post a Comment