Jumuiya ya Wazanzibar Nchini MAREKANI yaguswa na Msiba wa Mzee ABOUD JUMBE
zadiaspora@gmail.com
215 459 4449
zadia.org
انا لله وانا اليه راجعون
TAARIFA
Jumuiya ya Wazanzibari Nchini Marekani (ZADIA), imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Mzee Aboud Jumbe Mwinyi.
Mzee Jumbe aliyewahi kuwa rais wa Zanzibar na Makamo wa Kwanza wa Rais wa Tanzania, atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika harakati za kuleta maendeleo visiwani Zanzibar.
Chini ya Uongozi wake, kwa mara ya kwanza Zanzibar ilipata katiba yake na hivyo kuanzishwa kwa Baraza la Wawakilishi kama chombo cha uwakilishi wa Umma na kutunga sheria.
Marehemu Jumbe alikuwa rais wa Zanzibar kuanzia mwaka 1972 kufuatia kifo cha rais wa kwanza wa Zanzinbar Marehemu Abeid Aman Karume.
Aidha kono wa pole makhasusi uwafikie wanafamilia ya Marehemu, tukimwomba Mwenyezi Mungu Mtukufu awape subira katika kipindi hiki kigumu cha msiba, na kumwomba Mola Mlezi amlaze marehemu mahali pema Peponi... Amin.
Omar H Ali, Mwenyekiti, ZADIA
Agosti 14, 2016
Post a Comment