Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ametoa miezi miwili
kwa mkandarasi wa kampuni ya M/s Jiangxi Geo-Engineering (Group) Corporation
anayejenga sehemu ya barabara ya Mangaka-Nakapanya yenye urefu wa Km 70.5
kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami.
Amesema
hayo wakati akikagua ujenzi wa barabara ya Tunduru-Mangaka-Mtambaswala
inayojengwa kwa kiwango cha lami yenye urefu wa Km 202.5 ambayo kukamilika kwakwe
kutafungua fursa za kiuchumi na kuunganisha mikoa ya Ruvuma, Mtwara na Lindi.
Amebainisha
kuwa Mpango wa Serikali ni kuwajengea watanzania miundombili bora
itakayowafikisha katika uchumi wa kati ifikapo 2025 hivyo haitamvumilia
Mkandarasi anayechelewesha kukamilisha ujenzi wa miradi mbalimbali inayotekelezwa
hapa nchini.
"Natoa
miezi miwili mkandarasi uwe umemaliza hii barabara, wananchi wa Mangaka na
Tanzania kwa ujumla wanahitaji kuanza kuitumia kwa ajili ya kuinua uchumi wa
Taifa", amesema Waziri Prof. Mbarawa.
|
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (wa kwanza kulia), akitoa
maelekezo kwa Mhandisi Mkazi wa Kampuni ya Aurecon Amei Limited, Eng. Mesfin Gebremariam
(katikati), wakati alipotembelea barabara ya Mangaka-Mtambaswala yenye urefu wa
KM 65.5 kuona maendeleo ya ujenzi wake.
Waziri
Mbarawa ameongeza kuwa Serikali itaendelea kutoa fedha kwa Makandarasi
wanaotekeleza miradi mbalimbali nchini hivyo lazima wajipange kumaliza kazi kwa
wakati na kuzingatia viwango vya ubora kulingana na makubaliano ya
mkataba.
Aidha
amesisitiza kuwa Serikali haitaingia mkataba mwingine kwa mkandarasi
yoyote ambaye hatakamilisha kazi kwa wakati kulingana na makubaliano.
Kwa
upande wake Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) mkoa wa Mtwara
Eng. Dotto John amemhakikishia Waziri Mbarawa kusimamia mradi huo ili ukamilike
kwa wakati na kuchochea maendeleleo ya Mikoa ya kusini.
"Wananchi
wamengojea kwa muda mrefu kukamilika kwa mradi huu ili uwe kichocheo cha
maendeleo hivyo ninakuhakikishia kuwa nitawasimamia kwa umakini makandarasi
ili wazingatie vigezo tulivyokubaliana kwenye mkataba", amesisitiza Eng.
Dotto.
Waziri
Prof. Mbarawa amekagua mradi wa ujenzi wa barabara ya
Tunduru-Mangaka-Mtambaswala yenye urefu wa km 202.5 inayojengwa kwa kiwango cha
lami ambapo kukamilika kwake kutafungua fursa za kiuchumi mikoa ya Kusini
ikiwemo kuiunganisha Tanzania na Msumbiji kwa lami kupitia daraja la umoja
lililoko Mtambaswala.
|
|
Mkandarasi wa Kampuni
ya M/S Jiangxi Geo- Engineering (Group) akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, kuhusu maendeleo ya ujenzi wa
Barabara ya Mangaka-Nakapanya yenye urefu wa KM 70.5.
|
|
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (wa kwanza kulia), akitoa
maelekezo kwa Mkandarasi wa Kampuni y a Synohydro Cooperation Limited anaejenga
Barabara ya Nakapanya-Tunduruwakati alipotembelea barabara ya Mangaka-Mtambaswala
yenye urefu wa KM 66.5 kuona maendeleo
ya ujenzi wake.
|
|
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akisalimia na wananchi wa
Tunduru, aliyesimama kushoto mwenye Kaunda Suti nyeusi ni Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Ndugu Juma Homera, baada ya kukagua barabara ya Tunduru-Nakapanya KM 66.5, Mkoani Ruvuma.
|
Post a Comment