( MAKALA ) Kupinga Utumikishwaji Watoto Sio Jukumu la Serikali Peke yake
Benjamin
Sawe-Maelezo
Utumikishwaji
wa watoto umekuwa ni tatizo kubwa duniani ambapo kutokana na tawkimu za
makadirio za mwaka 2000-2012 za Shirika la Kazi Duniani asilimia 11 (watoto
milioni 264) ya watoto wote duniani wenye umri wa miaka 5-17 wnatumikisahwa
kwenye ajira za aina mbalimbali sawa na asilimia 11 ya watoto wenye umri huo.
Kwa
upande wa Tanzania, utumikishwaji wa watoto kwa mwaka 2014/15 matokeo ya
utafiti yanaonesha kuwa kati ya watoto milioni 15 wenye umri kati ya miaka 5
hadi 17 (watoto milioni 4.2) sawa na asilimia 28.8 wanatumikishwa katika kazi
mbalimbali.
Takwimu
hizo zinaonesha kuwa sekta za kilimo na uvuvi zimeendelea kuwa sekta
zinazoajiri watoto wengi zaidi ikiwa ni kiwango cha asilimia 92.1 ya watoto
wote wanaojihusisha na shughuli za kiuchumi na wengi wao wanaishi vijijini.
Akizungumza
katika uzinduzi wa ripoti ya matokeo ya utafiti wa utumikishwaji wa watoto
Tanzania Bara wa mwaka 2014, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt.
Albina Chuwa anasema matokeo ya utafiti huo yanaonesha kuwa watoto hutumia
zaidi ya nusu ya muda wao wa siku ikiwa ni asilimia 58.8 kwa shughuli za
kujihudumia na usafi huku wasichana wakionekana kutumia muda mrefu zaidi kwa
shughuli hizo kwa kiwango cha asilimia 58.3.
Ripoti
hiyo inaendelea kuonesha shughuli za kujisomea kwa watoto zilichukua nafasi ya
pili kwa matumizi ya muda kwa kiwango cha asilimia 15.5 ambapo wavulana
wanatumia muda mrefu zaidi kwa shughuli za kujisomea ikiwani sawa ana asilimia
16.4 ikilinganishwa na wasichana waliotumia wastani wa asilimia 14.6.
Dkt
Chuwa anasema matokea hayo yakilinganishwa na nchi nyingine za Afrika kama
Ghana yanaonesha kuwa watoto wa Kighana wenye umri wa miaka 10 hadi 17
wanatumia muda mwingi (asilimia 60.9) kwa siku kwenye shughuli za kujihudumia,
usafi binafsi na starehe kama kuangalia runinga ikilinganishwa na asilimia 23.4
ya muda wao kwa siku kwenye shughuli za kujisomea.
Akizindua
ripoti ya matokeo ya utafiti wa utumikishwaji wa watoto Tanzania Bara wa mwaka
2014, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Watu wenye ulemavu Mh. Dkt. Abdallah Possi (Mb) anasema Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania imesharidhia mikataba mbalimbali ikiwemo ya kikanda na
kimataifa inayohusiana na ustawi na haki za watoto.
Dkt.
Possi anasema mikataba iliyoridhiwa ni pamoja na Mkataba Na. 138 wa Shirika la
Kazi Duniani unaohusu umri wa chini unaoruhusiwa kujihusisha na ajira ya mwaka
1998 ambapo Mkataba na 182 wa utumikiswhaji wa watoto katika kazi hatarishi wa
mwaka 2002 unatafsiri mtoto kama mtu mwenye umri chini ya miaka 18.
Aidha
Tanzania imeridhia Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa mwaka 1989 unaohusu Haki za
Mtoto mwaka 1991, pia Serikali ilitunga Sheria ya Ajira na Mahusiano ya Kazi
Na. 6 ya mwaka 2014 inayozuia kuajiri watoto wenye chini ya miaka 14 ambapo
sheria hiyo inapiga marufuku kumfanyisha kazi mtot kwenye mazingira hatarishi
yanayoweza kuidhuru afya yake.
Kwa
mujibu wa Shirika la Kazi Duniani, utumikishwaji wa watoto unatafsiriwa kama
ushiriki wa watoto katika kazi zinazomnyima mtot haki yake ya utoto, utu na
fursa ya kujiendeleza ambazo pia huathiri watoto kiafya, kiakili, kielimu na
kijamii.
Kama
ilivyobainishwa katika Mkataba Na. 138 wa Shirika la Kazi Duniani, umri wa
chini wa mtoto kujihusisha na ajira ni miaka 15 au 14 kutokana na muundo wa
elimu ya msingi ya nchi husika.
Kwa
mujibu wa Ripoti ya Shirika la Kazi Duniani (ILO) kuhusu makadirio ya mwenendo
wa utumikishwaji wa watoto duniani ya mwaka 2000-2012 inaonesha karibu nusu ya
watoto wote wanaotumikishwa kwenye kazi mbalimbali, watoto milioni 85
wanatumikishwa kwenye kazi hatarishi (Hazodous Works) ambazo zinaathiri afya
zao, usalama pamoja na makuzi yao.
Kutokana
na tafiti hiyo utumikishwaji wa watoto wa mwaka 2014 Tanzania Bara umebaini
kuwa, kuna idadi ya watoto milioni 15 wenye umri kati ya miaka 5-17 ambapo kati
yao wavulana ni milioni 8 na wasichana ni milioni 7 na kundi kubwa la watoto ni
wenye umri wa miaka 5-11 wakiwa ni asilimia 59.6 ya watoto wote ikifuatiwa na
watoto wenye umri wa miaka 14-17 ambao ni asilimia 24.6.
Mgawanyo
wa kijinsia wa watoto wanaojihususha na ajira kwenye sekta ya kilimo unaonesha
kuwa wavulana ni asilimia 94.3 ya wavulana wote na wasichana ni asilimia 89.6
ya wasichana wote.
“Utumikishwaji
wa watoto umekuwa ni tatizo kubwa duniani ambapo nchi mbalimbali ikiwemo
Tanzania zinafanya jitiada za kutokomeza tazizo hili”Anasema Dtk. Possi.
Aidha
matokeo ya utafiti wa utumikishwaji wa watoto wa mwaka 2014 yanabainisha kuwa
kati ya watoto milioni 15 wenye umri kati ya miaka 5-17, watoto milioni 4.2,
sawa na asilimia 28.8 wanatumikishwa katika kazi mbalimbali za kiuchumi hapa
nchini.
Hata
hivyo mwenendo wa utumikishwaji wa watoto umepungua kutoka asilimia 31.1 mwaka
2006 adi asilimia 28.8 mwaka 2014.
Kutokana
na takwimu utafiti huo matokeo yanaonesha kuwa hali ya utumikishwaji wa watoto
imekuwa ikiongezeka kadri umri unavyoongezeka ambapo watoto wenye umri wa kati
ya miaka 14 hadi 17 wameonesha kuwa na kiwango cha juu cha asilimia 40.7
ikifuatiwa na watoto wenye umri wa miaka 12-13 sawa na asilimia 36.0 na miaka
5-11 sawa na asilimia 22.1.
Kwa
mgawanyiko wa kijiografia, matokeo yanaonesha kuwa tatizo la utumikishwaji wa
watoto ni kubwa zaidi katika maeneo ya vijijini kwa asilimia 35.6 ikilinganishwa
na maeneo ya miji mingine kwa asilimia 18.0 na Dar es Salaam kwa asilimia 3.6.
Utafiti
huo unebainisha kuwa jumla ya watoto milioni 10.2 wenye umri wa miaka 5 hadi 17
wanahudhuria masomo shuleni, miongoni mwao wavulana ni milioni 5.2 sawa na
asilimia 50.9 na wasichana ni asilimia 5.0 sawa na asilimia 49.1.
Akizungumza
hivi karibunu katika uzinduzi wa ripoti hiyo Dtk Possi anasema Serikali
itaendelea kupambana vikali na kupinga utumikishwaji wa watoto nchini na
kuhakikisha kuwa kiwango cha asilimia 28.8 kinapungua kwa kiasi kikubwa.
Dtk
Possi anasema moja ya jitihada zilizofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano
kupambana na utumikishwaji wa watoto ni kuanzisha programu ya ELIMU BURE ili kuhamasisha mahudhurio
ya watoto shuleni na kupunguza uwezekano wa watoto kujihusisha na ajira za
utotoni.
“Natoa
wito kwa wazazi na walezi kutumia vyema fursa ya kuwapeleka watoto shule ili
kuwaondoa katika janga la utumikishwaji wa kuzuia mimba za utotoni.
Aidha
anawaomba Shirika la Kazi Duniani (ILO) kuendelea kushirikiana na Ofisi ya
Taifa ya Takwimu kufanya uchambuzi zaidi wa kitaaluma ili kupata makadirio ya
viwango vya utumikishwaji wa watoto katika ngazi za chini kama vile mkoa ili
kudumusha hali halisi ya utumikishwaji wa watoto katika maeneo hayo.
Post a Comment