Chadema Nyanda za Juu Kusini na Nyasa Wasema Wapo Tayari Kwa UKUTA
Bw Frank Mwaisumbe.
CHAMA
cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Nyanda za Juu
Kusini (Nyasa) wameunga mkono maazimio
yote yaliyotolewa na kamati kuu cha Chadema chini ya mwenyekiti wake Taifa Bw
Freeman Mbowe ya
kuazisha oparesheni UKUTA .
Taarifa iliyotolewa
kwa vyombo vya habari leo na
mwenyekiti wa kanda ya nyanda
za juu kusini Bw
Frank Mwaisumbe alisema wamepokea
kwa mikono miwili maamizimio hayo
ya kuanzisha oparesheni
UKUTA nchini nzima
na kuwa wapo tayari
kwa kushiriki .
“Kwa ujumla wake (Mkoa wa Mbeya, Songwe, Rukwa, Iringa na
Njombe) inaunga mkono maazimio ya Kamati kuu ya Chama Chetu iliyoketi tarehe
27/07/2016 ya kupinga vikali aina zote za udikteta zinazoendelea na kufanywa na
serikali ya chama cha Mapinduzi (CCM)….. na kuwa tupo tayari kuona Demokrasia
ya vyama vingi nchini Tanzania inaendelea kuimarika kama iliyo asisiwa na Baba wa Taifa Mwal. Julius kamabarage
Nyerere, ambayo aliiacha ikiwa na amani na utulivu na kuwa nchi yenye kuruhusu
mfumo wa vyama vingi”
Alisema kuwa kwa
kuwa Tanzania ni moja kati ya
nchi zinazoendeshwa kwa
mfumo wa
vyama vingi ni
vema chama tawala CCM
kuacha kufinyanga Demokrasia hiyo na kuviacha
vyama vyote kufanya
kazi ya kujiimarisha kwa
uhuru na amani badala ya kuzuia
vyama kuendesha mambo yao .
Kwani alisema
ili chama kiwe
imara na chenye
nguvu ya kuleta
ushindani ni lazima kuwekeza
kwa wananchi na hivyo kuanzishwa kwa oparesheni UKUTA kutasaidia Chama
chao kuwekeza kwa wananchi kazi
ambayo hata CCM wamekuwa wakiendelea kuifanya
hadi sasa .
Mwaisumbe alisema
utakuwa ni uonevu mkubwa
iwapo serikali ya CCM itazuia
Chadema kuendelea na
Oparesheni UKUTA wakati juzi Dodoma katika Uwanja
wa Jamhuri aliyekuwa mwenyekiti
wa CCM Taifa Rais Mstaafu
Dr Jakaya Kikwete
alifanya mkutano mkubwa
ambao kimsingi si mkutano wa kiserikali ila ulikuwa ni mkutano wa Chama.
Alisema siasa safi
ni pamoja na kuruhusu vyama vyote
kuendelea ujenga vyama vyao ikiwa
ni pamoja na kutawaliwa na uhuru wa kuongea na uhuru wa kukosoa bila kuvunja
katiba ya nchi.
Bw Mwaisumbe alisema
wao kama Chadema kanda ya Nyasa watahakikisha wanafanya
zoezi hilo la Oparesheni UKUTA
pasipo kuvuruga amani ya
nchi na kuona mikutano yao
yote inafanyika kwa uhuru na
amani na wapo tayari
kuendelea kulinda amani na
utulivu.
“ sisi CHADEMA kanda ya Nyasa kwa pamoja tunajiunga na UKUTA Umoja
wa Kupinga Udikteta Tanzania.. wa UKAWA na tupo tayari wakati wote kupambana na
mtu yeyote anayevunja katiba na kuweka udikteta…. hii ni nchi yetu sote na
tupewe uhuru kwa usawa bila kuvunja katiba ya nchi”
Post a Comment