Mahakama Kuu Kanda ya IRINGA imemtia Hatiani Muuaji wa DAUDI MWANGOSI
Ulinzi wa polisi viwanja vya mahakama kuu kanda ya Iringa leo kabla ya mtuhumiwa wa mauaji kufikishwa.
Wananchi wakiwa foleni kukaguliwa kabla ya kuingia mahakamani leo.
Mtuhumiwa wa mauwaji ya Mwangosi akipakiwa kwenye gari za FFU.
Msafala wa gari za FFU zilizomsindikiz askari mwenzao anayekutwa na kosa la kuua bila kukusudia leo.
Askari wa FFU wakitoka mbio mahakamani hapo.
Wananchi na wanahabari wakitoka mahakamani hapo.
wakili
kutoka mtandao wa watetezi wa haki za
binadamu ((THRDC)Benedict Ishabakaki akizungumza na wanahabari nje ya viwanja vya mahakamani leo.
wakili
kutoka mtandao wa watetezi wa haki za
binadamu ((THRDC)Benedict Ishabakaki akizungumza na wanahabari nje ya viwanja vya mahakamani leo.
Siku ambayo mwanahabari Daudi Mwangosi alipouwawa.
Askari hao wakimtoa mahakamani hapo leo mtuhumiwa wa mauwaji ya Mwangosi.
Marehemu Mwangosi enzi za uhai wake.
MAHAKAMA kuu kanda
ya Iringa imemtia hatiani kwa
kosa la kuua bila kukusudia
askari Polisi Kikosi cha Kutuliza
Ghasia ( FFU )Iringa G 58 Pacificius
Cleophace Simon (27) anayetuhumiwa kuuua
mwaahabari Daudi
Mwangosi mwaka 2012 katika kijiji
cha Nyololo wilaya ya
Mufindi.
Huku wakili upande
wa jamhuri katika kesi
hiyo Adolph Mwaganda akiiomba
mahakama hiyo kutoa
hukumu ya kifungo
cha maisha jela kwa askari
huyo ambae hata hivyo
alisema upande wa jamhuri hauna
taarifa za makosa yoyote
aliyopata kuyafanya.
Hata hivyo mahakamani
hiyo imesema adhabu
kwa mtuhumiwa huyo
kutokana na kupatikana na kosa
hilo la kuua bila kukusudia
itatolewa Julai 27 majira ya
saa 4 asubuhi mwaka
huu.
Jaji Dkt Paul Kiwelo ambaye anayesikiliza
kesi hiyo alisema mahakakamani hapo leo kuwa kati
ya vielelezo vitano vyote
vilivyoleta kama ushahidi
mahakamani hapo kwa ajili ya
kesi hiyo namba 54 ya
mwaka 2013 ni kielelezo
kimoja pekee cha
ungamo kwa mlinzi
wa amani ambacho ndicho
hakukuwa na shaka na ungamo
hilo ndilo lililomtia hatiani asikari
huyo.
Alivitaja vielelezo
vilivyopelekwa kama ushahidi kuwa ni Ramani ya
eneo la tukio,ripoti ya
tabibu ,ungamo la mlinzi wa amani ,silaha aliyoitumia
na rejista ya
silaha .
Hata hivyo alisema
kuwa idadi ya
mashahidi katika kesi sio
inayowezesha kumtia hatiani
mtuhumiwa ila kinachomtia
hatiani ni aina ya ushahidi wenye uhakika ambao
unatolewa na kuongeza kuwa katika
kesi hiyo upande
wa jamhuri ulishindwa
kuleta mashahidi stahiki zaidi
ya kuwa na mashahidi ambao ukiacha mlinzi wa amani mashahidi
wote ushahidi wao una masahaka na haoonyeshi kama mtuhumiwa huyo
ndio aliyehusika na mauwaji .
“ Niseme baada ya kusikiliza
ushahidi wote …..mtuhumiwa
kaonekana na kosa la kuua ila kujua kama alikuwa na
nia ovu ama bila kukusudia ni jukumu la Jamhuri ambayo
ilipaswa kuleta ushahidi …..
maelezo ya ungamo ambayo
hata hivyo hayaonyeshi
alipanga ila ni uzembe
wa hali ya juu …..haijathibitika
kuwa alikusudia mahakama inaamini hakukusudia”
Hivyo alisema kuwa mahakama
yake imelifuta kosa la kuua
kwa kukusudia na
kumtia hatiani kwa
kosa la kuua bila kukusudia alisema jaji
Kiwele kuwa hamakama yake inashangazwa na RCO kwa
kuleta mahakamani kesi ambayo ushahidi wake
haukukamilika .
“ Ushahidi pekee ambao
ni ule wa mlizi wa amani hakimu Flora Mhelela ambae kweli
alitoa ushahidi usio
na shaka hata kidogo
ila ushahidi mwingine
wote ulikuwa na mashaka mengi
mfano ushahidi namba
moja , mbili na nne
ni ushahidi ambao
haukuwa halisi “.
Alisema mfano jambo la kujiuliuza katika ungamo lake
mtuhumiwa lisema kuwa silaha
aliyokuwa akitumika wakati
amemzingira mwanahabari huyo ilifyatuka bahati mbaya
hivyo ilikuwa ni mbovu ila
cha kushangaza hakuna hakuna
ushahidi unaoonyesha kuwa silaha
hiyo ilikuwa mbovu ama nzima.
Alisema kuwa si salama sana kumtia hatiani mtuhumiwa
huyo kwa kosa la mauwaji ya
kukusudia wakati upande wa jamhuri
umeshindwa kuleta ushahidi kamili unaoonyesha
kuwa mtuhumiwa huyo alikusudia
kufanya mauwaji hayo.
Aidha alisema mbali ya
upande wa utetezi
pamoja na mtuhumiwa kukana
ungamo alilolitoa Septemba 5
mwaka 2012 kwa mlinzi wa amani
kuwa hakulitoa kwa uhuru na amani
ila bado haisaidii kulikataa sasa maana
kama si kweli alipaswa
kielelezo hicho kukataliwa siku ya kwanza
kilipofikishwa mahakamani hapo kama
ushahidi hivyo mahakama hainashaka
na kieelezo hicho amacho
ni ungamo kwa mlinzi
wa amani.
Simon ambae
anatetewa na wakili wake Lwezaula Kaijage aliiomba mahakama
hiyo kutoa adhabu
sahihi yenye jicho la
huruma kwa mteja
wake huyo kwani hana wazazi
na yeye ndio anategemewa na wadogo
zake watano pia ana mtoto
wa miaka mitano anayehitaji zaidi malezi
yake katika makuzi yake.
“Mheshimiwa
jaji huyu mshitakiwa ni
kijana mdogo mwenye miaka 27
na ni nguvu kazi ya Taifa
pia katika oparesheni hiyo ya
Septemba 2 mwaka 2012 alikuwa katika kazi hiyo ambayo
ilikuwa ni amri ya jeshi na
kuwa slaha ililipuka
bahati mbaya basi
ijulikane hivyo pia
amekuwa mahabusi miaka minne na
kwa kipindi chote
amekuwa akijutia kosa lake hilo….
Naomba anachiwe huru
kwa masharti ambayo mahakama
inaona yanafaa”.
Huku wakili upande
wa jamhuri katika kesi
hiyo Adolph Mwaganda akiiomba
mahakama hiyo kutoa
hukumu ya kifungo
cha maisha jela kwa askari
huyo ambae hata hivyo
alisema upande wa jamhuri hauna
taarifa za makosa yoyote
aliyopata kuyafanya.
“ Hatuna kumbukumbu ya kosa lolote
ila kwa kuwa
mahakama imemtia hatiani kwa
kosa dogo la kuua bila
kukusudia tunaomba mahakama
yako kutoa adhabu kwa mujibu wa
kifungu namba 198cha kanuni
ya adhabu sura namba 16 mapitio ya
mwaka 2002 kwamba mtu yeyote aliyetiwa hatiani kwa
kosa la mauwaji ya bila
kukusudia afungwe jela
maisha “
Kesi hiyo ambayo ilijaza umati
mkubwa wa wakazi wa mji wa
Iringa huku polisi
wa FFU na wale
wa kawaida wakitanda nje ya
mahakama hiyo na ndani ya
chumba cha mahakama kabla ya
msajili wa mahakama hiyo kutoa onyo
kwa jeshi la
polisi kufuatia vurugu mbali
mbali wanazozifanya mara kwa mara katika
kesi hiyo , wakili kutoka mtandao wa
watetezi wa haki za binadamu ((THRDC)Benedict
Ishabakaki alisema
kuwa hajapendezwa na nguvu
kubwa ya jeshi la
polisi ambayo wanaitumika katika
kasi hiyo ndani
na nje ya mahakama
kuwa kinachofanyika ni kuingilia uhuru wa mahakama.
Kwani
alisema mahakama haipaswi kuingiliwa na chombo kingine
chochote na kuwa kitendo
cha polisi kuzuia wanahabari ndani ya mahakama
kufanya kazi zao kabla ya kesi kuanza ama
baada ya kesi kumalizika
si haki .
Lakini pia wakili msom I Ishabakaki,
alisema kwa maoni yake anaona kulikuwa
na mapungufu kwanzia kweye uchugunzi wa kesi ya mpaka uendeshaji wa kesi hiyo.
Wakili msomi alisema anaunga mkono maswali ambayo mahakama ilijiuliza kwa nini
RPC na RCO hawakuitwa kutoa ushaidi.
Wakili
anasema kutkana na mwenendo wa kesi kwa kitendo cha viongozi wa juu kutokuita
mahaakamani kuisaidia mahakama kunaweza kukawa kumepindisha haki sit u kwa
marehumu mwangosi lakini hata kwa askari
aliyehukuiwa.
Hii ni kutokana na kwamba mahakma iisema imepata kazi sana
kutambua siku hiyo oda ilitoka kwa nani.
Post a Comment