( MAKALA ) Lishe Bora Itasaidia Kupunguza Udumavu Kwa Watoto Ifikapo 2025
Na, Baraka Ngofira
Kila
kuchapo serikali na mashirika mbalimbali uangaika kutafuta suluhu juu ya
majanga mbalimbali ya udumavu wa watoto unaochangiwa na lishe duni wanazozipata
watoto katika umri chini ya miaka mitano.
Vikundi
mbalimbali na watu binafsi nao wamekuwa mstari wa mbele katika kuhamashisha
afya bora kwa kila mtu, juhudi hizi pia zinaungwa mkono na dini zote ambazo
usisitiza ulaji wa vyakula vinavyojenga na kuimalisha afya za waumini wao.
Lakini
bado hali ni tete hasa kwa watoto ambao wamekuwa wahanga wakubwa wa tatizo hili
ambapo udumavu na ukondefu unaosababishwa na kukosa lishe bora uchangia kwa
kiasi kikubwa kuwaathiri.
Takwimu za shirika la
Afya Duniani WHO, zinaonyesha kuwa kila siku zaidi ya watoto 270 walio chini ya
umri wa miaka mitano nchini Tanzania hupoteza maisha kwa lishe duni, huku zaidi
ya watoto milioni mbili na laki saba wakikabiliwa na udumavu unaotokana na
utapiamlo.
Hali ni mbaya zaidi kwa
kutokana na zaidi ya asilimia 40 ya vifo hivyo hutokea katika mwezi wa kwanza
wa maisha ya watoto hao. Pia kwa mujibu wa takwimu za shirika la Umoja wa Mataifa kwa shabaha ya kuwasaidia watoto duniani UNICEF, zinaonyesha
kuwa zaidi ya asilimia 42 ya watoto wote wa Tanzania waliochini ya umri wa
miaka mitano wamedumaa kutokana na lishe bora.
Katika
makala hii tutaangazia jinsi udumavu unavyochangia kwa kiasi kikubwa kuporomoka
kwa afya za watoto hali inayopelekea watoto kuwa na afya duni na utapiamlo.
Udumavu
hutokana na utapiamlo unaosabibishwa na lishe duni kwa mtoto ambapo huchangia
mtoto kuwa na kimo au urefu mfupi usioendana na umri wake.
Takwimu
hizo zinaonyesha kupungua kwa kiwango cha udumavu nchini kwa asilimia 30, kati
ya mwaka 1994 hadi 2014 japo idadi ya watoto waliodumaa ikiwa imeongezeka
kutoka milioni 2.4 hadi 2.7 katika kipindi hicho.
Wataalam
wa afya wametaja sababu kadhaa zinazochangia udumavu wa watoto nchini ambapo
lishe duni na kuugua mara kwa mara katika miaka mitatu ya mwanzo ya maisha ya
mtoto uchangia mtoto huyu kudumaa kimwili na kiakili pia.
Pia,
afya na lishe duni kwa wanawake kabla ya ujauzito, wakati wa ujauzito na baada
ya kujifungua. Wanawake kuwa na kimo kifupi, kutopangilia uzazi na hivyo kuzaa
karibu karibu na tatizo la wasichana kubeba mimba wakiwa katika umri mdogo nalo
linatajwa kuwa tazizo lingine linalosababisha na kuchangia udumavu nchini.
Taratibu
duni za ulishaji watoto wachanga na wadogo, ikiwemo watoto kutonyeshwa maziwa
ya mama kwa pekee katika kipindi cha miezi sita ya mwanzo baada ya kuzaliwa, na
kupewa chakula cha nyongeza kisichokidhi mahitaji yao ya kilishe pale
wanapotimiza umri wa miezi sita.
Kwa
kufanya hivyo na kupewa kiasi kidogo cha chakula, kupewa chakula kisichokuwa na
ubora na kutopewa chakula chenye mchanganyiko wa makundi mbalimbali ya chakula
napo uchochea udumavu kwa mtoto ambapo kwa kiasi kikubwa mwili wake na umri
wake hudumaa jambo linalochangia udumavu wa akili pia kwa mtoto huyo.
Athari za udumavu
Udumavu
kwa mtoto huchangia kupata athari zisizoweza kurekebishwa katika maisha yake na
daima atadumu nazo katika maisha yake yote hata kama kwa hapo baadaye hatapata
lishe bora lakini mwili wake tayari ushadumaa na hivyo ni vigumu kukubali
marekebisho.
Pia
udumavu kwa kiasi kikubwa husababisha kupungua kwa kasi ya maendeleo ya ukuaji
wa akili ya mtoto hali inayosababisha watoto kupata matokeo duni kielemu
kutokana na lishe bora waliyoipata wakiwa wadogo.
Lakini
pia kuongezeka kwa uwezekano wa watoto waliodumaa kuwa na uzito uliowazidi au
kiribatumbo, na kuugua magonjwa yasiyo ambukiza ikiwemo moyo, kiharusi,
shinikizo kubwa la damu, na kisukali wakati wanapofikia umri wa utu uzima nalo
utokana na ukosefu wa lishe duni walioipata wakiwa wadogo.
Maendeleo
ya ukuaji wa mtoto kimwili nao kuwa
dhaifu uchangiwa na upatikanaji wa lishe duni hali inayosababisha mtoto kuwa na
afya duni na mwonekano mbaya (body structure) ya mtoto hivyo mtoto kuwa na
mwili afya duni kutokana na mwili wake kutokuwa nguvu ya kupambana na magonjwa
nyemelevu ikiwemo minyoo, kuhara, typhod na mengine mengi.
Nini kifanyike ili kuzuia udumavu
nchini?
Lengo
kuu la Shirika la Afya duniani kwa Tanzania ni ifikapo mwaka 2025 walau idadi
ya watoto wenye umri chini ya miaka mitano waliodumaa iwe imepungua kwa walau
kwa asilimia 40. Hivyo ni muhimu kwa jamii ya watanzania kuzingatia lishe bora
kwa watoto na mama mjamzito na kulinda afya yake katika kipindi chocho cha
mimba hadi katika kipindi cha unyonyeshaji.
Ni
jukumu la kila mmoja kuhakikisha kuwa wanawakuwa katika hali nzuri ya lishe
wakati wa ujauzito na wakati wa kunyonyesha baada ya kujifungua hii itasaidia
kupunguza au kuondoa kabisa kero hii ya udumavu kwa watoto wa kitanzania ambao
ni taifa la kesho naa hapo baadaye watakuwa viongozi bora katika nchi hii na
duniani kiujumla.
Ni
muhimu kwa wakina mama kunyonyesha watoto wao maziwa hadi watakapofikia miaka
miwili, hapa wanaawake wajitahidi na waache uzembe wa kuwaachisha watoto wao
mapema kwa kisingizio au kuona aibu kunyonyesha. Ni muhimu kwa kila mzazi kwa
kushirikiana na familia yake kuwa mtoto ananyonya kwa kipindi cha miaka miwili
bila kuachishwa.
Pia
ni muhimu kuhakikisha kuwa watoto wananyonyeshwa maziwa ya mama pekee, bila
kupewa, vinywaji, au vyakula vingine katika kipindi cha miezi sita ya mwanzo
baada ya kuzaliwa. Ni muhimu kwa watoto wenye umri wa miezi 6 hadi 23 kupewa
chakula cha nyongeza vilivyo na ubora wa lishe.
Pia
ni lazima jamii ione umuhimu wa kuwakinga watoto na maradhi pamoja na kupatiwa
tiba ya magonjwa ya kuambukiza mapema mara tu, wauguapo maana jukumu la ulinzi
dhidi ya mtoto ni jukumu letu sote kama jamii na umma wote kiujumla.
Hivyo
basi tuone umuhimu wa kujenga taifa letu kwa kuzingatia lishe bora ili ifikapo
mwaka 2025, tuwe tumepunguza idadi ya watoto wenye umri chini ya miaka mitano
waliodumaa kwa asilimia 40 na hii itawezekana ikiwa tu kila mtu atafanya kwa
upande wake.
Kwa
mawasiliano wasiliana nami kwa simu namba 0763580901 au barua pepe ya
barakangofira@gmail.com
Post a Comment