Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amezungumzia umuhimu wa wananchi
wa mjini na vijijini kutumia simu ili waweze kunufaika na huduma mbalimbali za
kimtandao zinazotumika hapa nchini.
Akizungumza mara baada
ya kufungua mkutano wa nne wa kimataifa wa chama cha kampuni za simu duniani
GSMA mobile 360, Prof . Mbarawa amesema Serikali imejipanga kuhakikisha
miundombinu ya mawasiliano ya simu inawafikia wananchi wote ili kuwezesha
kunufaika na huduma za simu za kisasa.
‘Ili wananchi waweze
kupata maendeleo kwa haraka na kunufaika
na fursa za kimtandao katika masuala ya elimu, biashara, kilimo, afya na ustawi
wa jamii kwa ujumla kunahitajika uwepo wa simu za kisasa zinazoweza kuruhusu
mifumo ya kimawasiliano’, Amesema Waziri Prof. Mbarawa.
|
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akifungua mkutano wa nne wa
Chama cha Kampuni za Simu Duniani, GSMA Mobile 360, jijini Dar es Salaam.
Ameitaja mifumo hiyo
kuwa ni Elimu Mtandao, Afya Mtandao, Biashara Mtandao, Kilimo Mtandao, Serikali Mtandao, Hali ya
Hewa Mtandao ambavyo kwa pamoja
vitamhudumia mwananchi kwa ubora na wakati.
Amesisitiza kuwa
serikali inashirikiana kwa karibu na kampuni
za mawasiliano ya simu ndani na nje ya nchi ili kuhakikisha huduma za
simu zinakuwa za uhakika na salama.
Serikali inaendelea
kuhakikisha kwamba mfuko wa Mawasiliano Vijijini unaendelea kunufaisha
watanzania na mkakati wa kuhakikisha umeme unafika vijijini unaimarika sambamba
na uwepo wa simu za kisasa za bei nafuu.
Takribani laini za
simu milioni 39.9 nchini zinatumika katika huduma mbalimbali na hivyo huchangia
uchumi wa nchi.
|
|
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akikata utepe kuashiria
ufunguzi rasmi wa mkutano wa nne wa Chama cha Kampuni za Simu Duniani, GSMA
Mobile 360 jijini Dar es Salaam.
Waziri Prof. Mbarawa
amesema Serikali ya Tanzania itaendelea kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji
ili kukuza sekta ya mawasiliano hapa nchini ambapo hadi sasa tayari kilomita
18,000/- za mkongo wa taifa wa taifa wa mawasiliano zimejengwa hapa nchini.
“Serikali itaendelea kudhibiti vifaa vya
mawasiliano visivyo na ubora ili visiingie nchini na hivyo kuhakikisha
watumiaji wa mitandao ya simu wanakuwa salama na wanaitumia mitandao hiyo kwa
wakati wote’, Amesisitiza Prof. Mbarawa.
Mkutano huo wa siku
mbili ambao pia umehudhuriwa na Naibu Waziri Mkuu wa Nchi ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo (DRC) Bw. Thomas Luhaka ambapo pamoja na mambo mengine
utajadili Changamoto mbalimbali na kuja na suluhisho na namna bora ya
kuendeleza Sekta ya Mawasiliano duniani.
|
|
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Profesa Makame Mbarawa, akishuka kwenye gari maalum la mawasiliano baada ya
kukagua mitambo mbalimbali ya Mawasiliano ya simu jijini Dar es Salaam. |
|
Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa nne wa Chama cha Kampuni za Simu
Duniani, GSMA Mobile 360, wakifatilia mada jijini Dar es Salaam.
|
Post a Comment