Sehemu
ya Makatibu Wakuu wa Wizara zinahusika moja kwa moja na ujenzi wa Bomba la
Mafuta na Wakuu wa Mikoa ambayo Bomba
hilo linapita kutoka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania
wakati wa semina ya siku moja juu ya ujenzi wa bomba hilo.
Profesa
Muhongo ametaja baadhi ya Wizara ambazo zina husika moja kwa na ujenzi wa bomba
hilo kuwa ni pamoja na Wizara ya Nishati na Madini, Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano
na Uchukuzi,Wizara ya Viwanda na Biashara, Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi
pamoja na Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Wizara
zingine ni pamoja na Wizara ya Mambo ya
nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais,
Mazingira, Pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii.
Mradi
wa ujenzi wa Bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga
nchini Tanzania utakuwa Mradi wa tatu kwa Ukubwa nchini Tanzania ukitanguliwa
na ule wa Ujenzi wa Bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Tanzania hadi
Zambia( TAZARA) na Ujenzi wa Bomba la Gesi kutoka Mkoa Mtwara hadi Jijini Dar
es salaam.
Bomba
hilo litakuwa na urefu wa kilomita 1,443 na upana wa nchi 12, litagharimu
shilingi bilioni 3.5 na unatarajiwa kukamilika mwaka 2020.
|
Post a Comment