Na Raymond Mushumbusi
Wasanii nchini wameaswa kuzingatia maaadili katika utengenezaji wa kazi zao ili kuenzi na kulinda mila, desturi na tamaduni za mtanzania.
Wito huo umetolewa jana na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura wakati akizindua studio ya kisasa ya kurekodi kazi za sanaa ya Wenene Entertainment.
Mhe Anastazia Wambura amesema kuwa baadhi ya wasanii wamekuwa hawafati maadili katika utengenezaji wa kazi zao na kuvifanya vyombo vinavyosimamia kazi za sanaa nchini kama Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kutoa adhabu dhidi yao kutokana na ukiukwaji wa maadili katika kazi zao.
“Ninaiomba kampuni ya Wanene Entertainment kuisaidia Serikali kuwaelimisha wasanii watakaoleta kazi zao kutengenezwa kwenu kuzingatia maadili badala ya kutengeneza kazi ambazo haziendani na maadili ya nchi yetu” alisema Mhe Anastazia.
|
Post a Comment