Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame
Mbarawa (wa kwanza kulia) akizungumza
kumshukuru Rais wa Benki ya Exim ya nchini China Bw, Liu Lian’ge (hayupo
pichani) mara baada ya kukagua kituo mahiri cha kutunza kumbukumbu (Internet
Data centre) kilichopo eneo la kijitonyama Dsm.
Kwa
upande wake Waziri Profesa Makame Mbarawa (Mb) ameipongeza Serikali ya China
kupitia Benki hiyo kwa kuwa wadau wakubwa wanaochangia fedha kwa ajili ya
maendeleo ya nchi na kuomba ushirikiano huo uwe endelevu kwa manufaa ya nchi
hizo mbili.
Naye,
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayesimamia sekta ya
Mawasiliano) Prof. Faustine Kamuzora amesema maendeleo makubwa kwenye ukuaji wa
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) yamesababisha uzalishwaji
mwingi wa data hivyo Serikali na Sekta mbalimbali wanahimizwa kutumia kituo
hicho mahiri cha kuhifadhia kumbukumbu zao kwani zitakuwa salama.
Amesema
huduma ya mtandao katika kituo hicho imeimarishwa kutokana na kuunganishwa na
mkongo wa taifa na hivyo itawarahisishia wateja wake kuweka na kuchukua taarifa
kwa haraka.
Kituo
cha kutunza Kumbukumbu (Internet Data Centre) ambacho ni cha kwanza
kujengwa katika nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ni fursa mpya kwa
wafanyabiashara na wadau mbalimbali wenye taarifa nyingi kuzihifadhi na
kuzitumia wanapozihitaji, kinalimikiwa na Serikali.
|
Post a Comment