Header Ads

MAN UTD V/S DORTMUND kufungua Pazia la michuano ya ICC



 IKIWA chini ya kocha wake mpya Mreno, Jose Mourinho, Manchester United wanatarajia kushuka dimbani jijini Shanghai, China kuwakabili Borrusia Dortmund siku ya Ijumaa Julai 22, 2016 mechi itakayopigwa saa tisa za alasiri kwa saa za hapa nyumbani.

Michuano hiyo itakuwa ni ya kusisimua kutokana na orodha ndefu ya timu kubwa zitakazoshiriki kama vile Real Madrid, Barcelona, Manchester United, Manchester City, Paris Saint-Germain, Juventus, Liverpool, Chelsea na Bayern Munich kwa uchache.

Mchezo huo ni sehemu ya ufunguzi wa michuano ya kombe la mabingwa wa kimataifa almaarufu kama International Champions Cup au ICC itakayoanza kutimua vumbi Julai 22 na kumalizika Agosti 13, 2016 katika viwanja mbalimbali nchini Marekani, Ulaya, Australia na China.

Katika michuano hii wapenzi wa soka duniani watapat fursa kujionea kwa mara kwanza mechi ya watani wa jadi kutoka jiji la Manchester au unavyojulikana kama ‘Machester Derby’ miongoni mwa mashabiki wengi. Mechi hiyo itapigwa siku ya Jumatatu ya Julai 25 jijini Beijing, China.

Mchezo huo utanogeshwa si tu na ushindani baina ya wachezaji au mashabiki bali safari hii ni makocha waliopewa vibarua vya kunoa vikosi hivyo, Jose Mourinho wa Manchester United na Pep Guardiola wa Manchester City.

Ukiachana na mechi hiyo, pia macho ya mashabiki wengi yatakuwa yakisubiria kwa hamu kutazama mechi kali zitakazozikutanisha timu za, Real Madrid na  PSG,  Chelsea na Liverpool, Real Madrid na Chelsea, Bayern Munich na Real Madrid pamoja na Liverpool na Barcelona.

Kwa ujumla timu zitazoshiriki  michuano hii ni pamoja na Real Madrid, Barcelona, Manchester United, Manchester City, Paris Saint-Germain (PSG), Juventus, Liverpool, Chelsea, Bayern Munich, Liverpool, Tottenham Hotspurs, AC Millan, Inter Millan, Leicester City FC, Celtic FC, Atletico Madrid, Melbourne Victoria na South China.


No comments

Powered by Blogger.