MADAWATI
745 ambayo yalitengenezwa na mfuko wa jimbo la Kilolo kwa gharama
ya Tsh milioni 30 zilizotolewa na mbunge wa jimbo hilo Venance
Mwamoto ambayo yalikataliwa na mbunge huyo na mkuu wa mkoa wa
Iringa Amina Masenza yamekamilika kutengenezwa kwa ubora .
Akizungumza
baada ya kukabidhiwa madawati hayo leo mbunge Mwamoto alisema
kuwa amekubali kupokea madawati hayo baada ya kufurahishwa na
ubora wake na hivyo imani yake kuona walimu wanasimamia
utunzaji wa madawati hayo ili kuondokana na kero tena ya madawati
katika shule zote za wilaya ya Kilolo.
Mbunge
Mwamoto alisema kuwa kufuatia uhaba wa madawati uliyokuwa
ukiikumba wilaya ya Kilolo na kama sehemu ya utekelezaji wa agizo
la Rais Dr John Magufuli alilazimika kuidhinisha pesa kiasi cha Tsh
milioni 30 kutoka mfuko wa jimbo la Kilolo ili kuweza kusaidia
utengenezaji wa madawati 300 japo Halmashauri ya Kilolo kupitia
wadau wake wa ndani na makusanyo ya ndani waliweza kuongeza kiasi
cha Tsh milioni 19 na kufanya kuwepo kwa kiasi cha pesa cha Tsh
milioni 49 ambazo zilifanikisha kutengeneza madawati zaidi ya 1000 .
Alisema
kuwa pamoja na kazi nzuri iliyofanywa na Halmashauri hiyo katika
kushughulikia kero ya madawati katika wilaya hiyo ya Kilolo ila
mafundi ambao walipewa kazi ya kutengeneza madawati hayo hawakuwa
wazuri kutokana na kushindwa kuifanya kazi hiyo kwa ubora uliotakiwa
hivyo kupelekea kufanya kazi hiyo kwa kiwango cha chini zaidi.
"Nililazimika
kukataa madawati 40 ambayo yalipelekwa shule ya Msingi Nyanzwa na
Igunda baada ya kuyaona hayana ubora na wananchi kulalamika kuwa
ni mabovu ukilinganisha na madawati ambayo yalitengenezwa kwa nguvu
ya wananchi katika vijiji hivyo ......hivyo sikuwa tayari kupokea
madawati hayo hali iliyopelekea mkuu wa mkoa wa Iringa kufika kuona
madawati hayo na kulazimika kuyakataa madawati yote 745 kwa kutaka
yatengenezwe kwa ubora"
Mwamoto
alisema kuwa amefurahishwa na usimamizi mzuri wa mkuu wa wilaya ya
Kilolo na timu yake ya mkurugenzi wa wataalam wengine ambao
wameweza kuifanya kazi hiyo ya kusimamia ubora kwa muda mfupi wa
wiki tatu kinyume na muda ule wa mwezi mmoja uliotolewa na mkuu wa
mkoa wa Iringa .
Hata
hivyo Mwamoto alisema kuwa yawezekana wapo watendaji ambao
walimchukia kwa yeye kukataa madawati hayo ila ukweli alifanya hivyo
kusaidia watoto wa wana Kilolo kutoendelea kukaa chini na kuwa iwapo
madawati hayo yangepelekwa shuleni bado wananchi wangebeba dhamana
ya kuendelea kuchangishana kwa ajili ya kuchonga madawati.
Kwa
upande wake mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah alisema kuwa
baada ya mkuu wa mkoa wa Iringa kumpa agizo la kusimamia zoezi
hilo ndani ya mwezi mmoja alilazimika kuifanya kazi hiyo kwa haraka
zaidi ndani ya wiki tatu ili kuona wanafunzi wote wanakaa kwenye
madawati .
Alisema
kuwa timu ya wakuu wa idaraka katika wilaya ya Kilolo wameonyesha
ushirikiano mkubwa katika kutekeleza agizo hilo na kuwa baadhi yao
walikuwa wanalala kwenye karakana zilizopewa kazi ya kutengeneza
madawati hayo mapema kabla ya muda waliopewa na mkuu wa mkoa wa
Iringa .
Wakati
mkuu wa mkoa wa Iringa Bi Masenza pamoja na kumpongeza mkuu wa
wilaya ya Kilolo na timu yake kwa kutekeleza zoezi la usimamiaji wa
ubora wa madawati hayo bado alimpongeza mbunge wa Kilolo Bw Mwamoto
kwa kubaini suala hilo huku akiwataka walimu katika shule zote
kuhakikisha wanatunza madawati hayo ili kuondokana na adha ya
kuchangia madawati mara kwa mara .
"
Nimeridhishwa na ubora wa madawati hayo na yale machache ambayo
yalipelekwa mashuleni wanaendelea kuyarekebisha ili yaweze kufanana
na haya ambayo kweli yapo katika ubora mzuri ".
TAZAMA VIDEO CHINI
|
Post a Comment