Muonekano
wa awali wa ujenzi wa Mabweni ya wanafunzi wa Chuo kikuu cha Dar es salaam.
Kwa upande wake Meneja
Miradi wa TBA Arch. Humphrey Killo amesema ujenzi wa mradi wa mabweni ya
wanafunzi utahusisha ujenzi wa vyumba 960 vyenye uwezo wa kuchukua jumla ya
wanafunzi 3,840 na ujenzi huo utakamilika ndani ya miezi sita.
Naye Mtendaji Mkuu wa
TBA Arch. Elius Mwakalinga amemhakikishia waziri kuwa wakala wake utafanya kazi
usiku na mchana ili kukamilisha kwa wakati mradi huo kwa kuwa inayo uwezo wa
kiteknolojia wa ujenzi wa miradi ya majengo hapa nchini.
"Kuonyesha kuwa
uwezo wa kufanya miradi kama hiyo tunayo, tutaikamilisha kwa wakati na viwango
stahili ili wateja wapate thamani ya pesa watakayolipa", amesema Arch. Mwakalinga.
Zaidi ya nyumba
10,000 za makazi ya watumishi wa umma zinatarajiwa kujengwa na kuuzwa
katika mradi wa Bunju "B" ikiwa ni mkakaati wa Serikali kuwawezesha
watumishi wa umma kupata nyumba bora kwa bei nafuu. |
Post a Comment