Na Immaculate Makilika- Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli amewaasa watanzania kudumisha amani iliyopo ambayo ilipatikana baada ya Mashujaa mbalimbali kuipigania na hata kujitoa uhai wao kwa ajili ya Taifa.
Akizungumza leo, wakati akihutubia wananchi mara baada ya kumaliza shughuli za maadhimisho ya Siku ya kumbukumbu ya Mashujaa iliyofanyika katika viwanja vya Mashujaa vilivyopo mjini Dodoma.
Rais Magufuli alisema kuwa maadhimisho ya kumbukumbu za Mashujaa ni muhimu kwa vile watu hao walijotoa kwa ajili ya kulitetea taifa.
“Wakati tunawakumbuka waliotangulia mbele za haki, sisi tuliobaki tudumishe amani hii, kama ambavyo wao waliotutangulia hawakujali dini zao bali taifa hili” alisema Rais Magufuli.
|
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiongea leo na
wakazi wa Dodoma na watanzania kwa ujumla wakati wa shughuli ya maadhimisho ya
Siku ya kumbukumbu ya Mashujaa Tanzania na kuwaasa watanzania kudumisha amani ambayo
ilipatikana baada ya Mashujaa wetu kuipigania na hata kujitoa uhai wao kwa
ajili ya Taifa.
|
|
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mheshimiwa Alhaji Ali Hassan Mwinyi akiongea leo
na wakazi wa Dodoma na watanzania kwa ujumla wakati wa shughuli ya maadhimisho
ya Siku ya kumbukumbu ya Mashujaa Tanzania na kuwataka watanzania kumuunga
mkono Mhe. Rais Dkt. Magufuli katika harakati za kuijenga Tanzania mpya.
Aliongeza kuwa nchi ya Tanzania imebaki kuwa kisiwa cha amani, na amani hiyo isichezwe bali ijengwe na kudumishwa kwa umoja na mshikimamano ili kusaidia kuitangaza nchi zaidi.
Aidha, viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mheshimiwa Dkt.Ali Mohamedi Shein, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mheshimiwa Alhaji Ali Hassan Mwinyi, Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa John Samweli Malecela nao wapewa fursa ya kuzungumza na wananchi kuhusu maadhimisho hayo ya kumbukumbu ya siku ya Mashujaa.
Viongozi hao, wamesisitiza umuhimu wa kudumisha amani iliyopo na kusema kuwa ni jukumu la wananchi wote kuhakikisha hawashiriki katika vitendo vitakavyosababisha uvunjifu wa amani.
Ambapo, waliwataka wananchi kuwaombea Mashujaa wote waliofariki katika vita mbalimbali wakiwa katika harakati za kulifanya Taifa la Tanzania kuwa huru.
|
|
Rais
wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mheshimiwa
Dkt.Ali Mohamedi Shein akiongea leo na wakazi wa Dodoma na watanzania
kwa ujumla wakati wa shughuli ya maadhimisho ya Siku ya kumbukumbu ya Mashujaa
Tanzania na kusisitiza kuhusu umuhimu wa watanzania kuenzi amani iliyoasisiwa
na wazee wetu na kuacha kushiriki katika vitendo vinavyoashiria uvunjifu wa
amani.
|
|
Waziri
Mkuu Mstaafu Mheshimiwa John Samweli Malechela akiongea leo na wakazi wa Dodoma na
watanzania kwa ujumla wakati wa shughuli ya maadhimisho ya Siku ya kumbukumbu
ya Mashujaa Tanzania na kumshukuru kwa kusimamia na kutekeleza ahadi zilizowahi
kutolewa na hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ikiwemo
kuhamishia serikali Mkoani Dodoma.
|
|
Waziri
Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa akiongea leo na wakazi wa Dodoma na watanzania
kwa ujumla wakati wa shughuli ya maadhimisho ya Siku ya kumbukumbu ya Mashujaa
Tanzania na kumuahidi Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuwa atahakikisha
anasimamia utekelezaji wa maagizo ya kuitaka Serikali ihamie mjini Dodoma.
Wakati huo huo, Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa, alisema kuwa atahakikisha anasimamia utekelezaji wa agizo la Rais la kuitaka Serikali kuhamia mjini Dodoma.
“Nahamia Dodoma mwezi wa tisa,na nitakapohamia mawaziri wote lazima wanifuate. Katika hili nitasimamia kwa nguvu zote” alisema Waziri Mkuu Majaliwa.
Awali, Mheshimiwa Rais Magufuli alisema kuwa atahakikisha katika kipindi cha utawala wake, Serikali inahamia mjini Dodoma, kwa vile Rais wa Awamu ya kwanza Mwl. Julius Nyerere alionesha nia ya kufanya hivyo.
Aliongeza kuwa kwa sasa mji wa Dodoma unaweza kukidhi mahitaji hayo ya Serikali kwa kutumia miundombinu iliyopo, hata hivyo Serikali inaendelea kujenga miundombinu mipya.
Maadhimisho ya kumbukumbu za Mashujaa hufanyika Julai 25, ya kila mwaka, kwa kufanya maombolezo ya Mashujaa waliopigana katika vita mbalimbali katika harakati za kutetea uhuru wa nchi ya Tanzania.
Maadhimisho ya mwaka huu yamefanyika kwa mara ya kwanza mjini Dodoma, ambapo Rais John Pombe Magufuli alikuwa mgeni rasmi, ikiwa ni mara yake ya kwanza kuhudhuria maadhimisho hayo kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
|
|
Mnara
wa Kumbukumbu ya Mashujaa baada ya kuwekwa kwa silaha za asili za mashujaa na
maua.
|
|
Baadhi
ya wananchi wakifuatilia shughuli ya maadhimisho ya Siku ya kumbukumbu ya
Mashujaa Tanzania katika viwanja vya Mashujaa vilivyopo mjini Dodoma.
(Picha na Hassan Silayo)
|
|
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika
viwanja vya Mashujaa vilivyopo mjini Dodoma wakati wa shughuli ya maadhimisho
ya Siku ya kumbukumbu ya Mashujaa Tanzania.
|
|
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiweka
silaha za asili kwenye Mnara wa Mashujaa leo Mkoani Dodoma wakati wa shughuli ya
maadhimisho ya Siku ya kumbukumbu ya Mashujaa Tanzania.
|
Post a Comment