Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amezitaka taasisi zilizo
chini ya Wizara yake kuanzisha mfumo maalumu wa makubaliano utakaotumika kupima
utendaji kazi wa watumishi ili kuweza kufikia malengo yaliyokusudiwa na kutoa
matokeo chanya.
Waziri Mbarawa
ameyasema hayo Mkoani Rukwa alipofanya mazungumzo na Viongozi na watendaji wa
taasisi hizo wakati alipotembelea mkoa huo kwa lengo la kukagua hali ya
miundombinu na kuwaeleza mtazamo mpya wa Serikali ya Awamu ya Tano.
Amesema katika
mfumo huo Waziri ataingia mkataba na wenyeviti wa bodi wakati Katibu Mkuu wa kila
sekta kuingia mkataba na watendaji wakuu wa taasisi hizo na watendaji hao
wataingia mikataba na wafanyakazi wao ili kuweza kuweka mazingira ya kila mfanyakazi
kufikia malengo yaliyowekwa na wizara pamoja na taasisi husika.
“Mimi
nitawekeana mkataba na wenyeviti wa bodi za taasisi zote, kwa Sumatra moja ya
vipengele vitakavyokuwa kwenye mkataba
huo ni pamoja na mkakati madhubuti wa kupunguza ajali za barabarani
zinazosababisha vifo kwa Watanzania, TCRA
Makusanyo kwenye makampuni ya simu na taaasisi nyingine hivyo hivyo”, amesema
Prof. Mbarawa.
|
Post a Comment