Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki
(Mb) (kulia) akisaini kitabu cha wageni Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, kabla
ya kikao kazi na watumishi wa mkoa wa Morogoro kilichofanyika tarehe 15/7/2016
katika ukumbi wa mikutano wa Manispaa ya Morogoro, Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa
Morogoro, Dkt. Kebwe Steven Kebwe na kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa
Morogoro, Mhandisi Dkt. John Ndunguru.
Amesema eneo la ofisi za Masijala
limekuwa likilalamikiwa kwa kiasi kikubwa kwa majalada kutoonekana na kusababisha
watumishi na wadau kutopata mrejesho.
“Tutoe mwongozo kwa watumishi
wa Masijala na tusiwaache bila kuwafuatilia kwani eneo hili limekuwa likilalamikiwa
sana. Ikiwezekana tufanye kaguzi za kushtukiza ili kuleta ufanisi katika kazi”
Mhe. Kairuki aliongeza.
Ameongeza kuwa ufuatiliaji
pia ufanyike kwa kila Ofisa ambaye anakaa na jalada kwa muda mrefu bila kutoa mrejesho.
Mhe. Kairuki amekutana na watumishi
wa Mkoa wa Morogoro ikiwa ni mwendelezo wa ziara alizozipanga kuzitekeleza mikoani
kwal engo la kusikiliza kero za watumishi ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi na kuangalia
ni namna gani ya kuweza kuboresha utendaji kazi Serikalini.
|
Post a Comment