Na Theresia Mwami - TEMESA
Ujenzi wa kivuko kipya cha Mv Pangani uko katika hatua za mwisho na kinategemea kumamilika Julai mwaka huu na kuanza kutoa huduma.
Hayo yamesemwa na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi. Lekujan Manase alipotembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa kivuko hicho ambao upo mbioni kukamilika kwa kuanza kutoa huduma kwa wananchi.
“Kivuko hiki kipo katika hatua za mwisho za ujenzi wake na leo tumekuja hapa kukagua mitambo ya kuendeshea kivuko (propulsion units) pamoja na injini zilizofungwa katika kivuko hiki ili kukamilisha ujenzi wake na hatimaye kianze kufanya kazi” alisema Mhandisi Manase.
|
Post a Comment