TRA yajivunia Kasi ya Ukusanyaji wa Kodi
ISO
9001:2008 CERTIFIED
TAARIFA YA MAKUSANYO YA KODI
Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) imekusanya jumla ya shilingi trililion 3.77 kuanzia mwezi Julai hadi Oktoba 2015 ambayo ni sawa na
asilimia 97.6. ya lengo la makusanyo ya sh trilioni 3.87 ikiwa ni jitihada za TRA kutekeleza mkakati wa serikali ambao
unaitaka kukusanya Ths . Trililioni 12.3
kwa mwaka wa fedha 2015/2016.
Kwa
mujibu wa Kamishna Mkuu wa TRA Rished
Bade, mwezi Julai TRA ilikusanya kiasi cha shilingi bilioni 849,582.9 ambacho ni asilimia 99.4 ya lengo la kukusanya shilingi
bilioni 854,922.9.
Mwezi
Agosti TRA ilikusanya kiasi cha shilingi bilioni 890,536.7 ambacho ni asilimia 101.5 ya lengo la kukusanya shilingi
biilioni 876,974.2 .ambapo mwezi Septemba jumla ya shilingi trilioni 1,067,888.3 zilikusanywa ikiwa ni
asilima 91.7 ya lengo trilioni 1,163,999.4
kwa mwezi mwezi Oktoba TRA iilkusanya
shilingi bilioni 970,089.6 ikiwa ni
asilima 99.3 ya lengo la kukusanya shilingi
bilioni 976,441.5.
Taarifa
ya mwenendo wa makusanyo ilipitishwa na Bodi ya Wakurugenzi ya TRA katika kikao
cha bodi kilichofanyika jana tarehe 10 Novemba 2015 katika ofisi za makao makuu
ya TRA” amesema Bw. Bade.
Mafanikio
katika makusanyo haya yametokana na mikakati madhubuti iliyowekwa na mamlaka
baada ya kusaini mkataba na Waziri wa Fedha ambapo Kamishna Mkuu alisaini
mkataba na kila Mkuu wa Idara na wakuu wa Idara kusaini mikataba na wafanyakazi
walioko chini yao ili kila mfanyakazi kuwajibika ipasavyo.
Wito
wa TRA ni kwa mfanyabiashara na wadau wote wa kodi kutimiza wajibu wao wa
kulipa kodi kwa hiari ili kuchangia pato la taifa.
Sambamba
na hilo TRA imepokea kwa furaha sana wito wa Mheshimiwa Rais John Pombe
Magufuli wa kuhimiza ukusanyaji wa mapato bila woga na bila kumwonea mtu.
“Pamoja
Tunajenga Taifa Letu”
Rished Bade
KAMISHNA MKUU
Post a Comment