Serikali yadaiwa Shilingi Bilioni 1.1 na Walimu..?
Amina Kisenge |
WALIMU wa Mkoa wa Dar es Salaam wanaidai Serikali jumla ya sh. Bilioni 1.1 za madai yao mbalimbali kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2013 hadi 2015.
Hayo yalielezwa na Mwenyekiti wa Chama cha Walimu (CWT) Mkoa wa Dar es Salaam, Mwalimu Amina Kisenge (pichani kushoto), katika kikao cha baraza la dharura la chama hicho lililoketi hivi karibuni.
Awali CWT ilikua ikidai jumla ya Sh.Bilioni 3.9 kabla ya kupunguza kiasi cha Sh.Bilioni 1.9 mapema mwaka huu.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti, madeni hayo ni pamoja na malimbikizo ya nauri za likizo kuanzia mwezi wa Juni na Desemba, 2013; na Juni na Desemba mwaka jana.
Malimbikizo mengine ni pamoja na pesa ya kuwasafirisha
wastaafu kwenda majumbani kwao, alisema Kisenge.
"Uhamisho wa walimu kutoa kituo kimoja kwenda kingine ikiwa ni posho ya usumbufu na ya kujikimu; pamoja na pesa za gharama za masomo baada ya walimu kujigharamia kujisomesha, imekuwa pia ni tatizo kwa serikali kutoa," alisema Mwenyekiti.
Kisenge aliongeza kwamba chamgamoto nyingine inayowakabili walimu ni mfuko wa PSPF kutowalipa walimu wastaafu kwa wakati ambapo walimu waliostaafu Januari hadi Septemba mwaka huu hawajalipwa mafao yao.
Kero nyingine kwa mujibu wa CWT ni walimu kutopandishwa madaraja kwa wakati na kwa wale wanaobahatika kupanda madaraja, mishahara yao hairekeshwi.
Wakati huohuo, CWT iliitaka serikali ya awamu ya tano kuharakisha matumizi ya chombo cha ajira kwa walimu kilichopitishwa na serikali ya awamu ya nne;kwamba chombo hicho ndicho mkombozi wao.
Post a Comment