Mahakama ya TANZANIA yafungua Milango kwa Wanahabari Nchini
Jaji Kiongozi wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Shaban Ally Lila akifunga Mafunzo ya siku mbili ya Waandishi wa Habari za Mahakama yaliyofanyika jijini Dar es salaam. |
Na Aron
Msigwa –MAELEZO
Mahakama
ya Tanzania imesema kuwa itendelea kufanya kazi na vyombo vya Habari nchini katika
kuuhabarisha umma kuhusu utekelezaji wa jukumu la Kikatiba ililonalo la kutafsiri
sheria mbalimbali na kuzitolea maamuzi ili kuwawezesha wananchi kujua na kupata
Haki zao kwa wakati.
Akifunga
Mafunzo ya siku 2 ya waandishi wa Habari za Mahakama jana jijini Dar es salaam Jaji
Kiongozi wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Shaban Ally Lila aliwataka waandishi hao kutimiza
wajibu wao wa kuueleza umma taarifa sahihi za mashauri mbalimbali yanayotokea
mahakamani kwa kuzingatia sheria.
Alisema
vyombo vya habari na mahakama vinahitajiana, vinafanya kazi pamoja kwa manufaa
ya umma huku akieleza kuwa mikutano ya mara kwa mara kati ya wanahabari na
mahakama kunaongeza kuaminiana na kujenga mahusiano mazuri.
Alifafanua
kuwa kazi ya Mahakama kikatiba ni kutafsiri sheria mbalimbali na kuzitolea
maamuzi kwa mujibu wa sheria kulingana na mashauri yananayowasilishwa
Mahakamani na kuongeza kuwa hakuna Jaji wa Mahakama ya Tanzania anayeamua kesi
bila nje ya utaratibu wa sheria zilizopo.
Alisema wao
kama majaji hutumia sheria zilizopo katika kutoa maamuzi hata kama
haziwapendezi wahusika na kuongeza kuwa jambo wanalolifanya ni kutoa maoni na
mapendekezo kwa mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa hatua zaidi.
" Sisi
kama Majaji hutumia sheria zilizopo kutoa maamuzi,hatutungi sheria jukumu letu
kikatiba ni kutafsiri sheria mbalimbali na kuzitolea maamuzi pia tunatumia
fursa ya maamuzi tunayoyatoa kuelimisha jamii kuhusu sheria iliyotumika kutoa
haki katika kesi husika" Alisema.
Aliwataka
waandishi wa Habari za Mahakama kujipa muda wa kutosha pindi wanapofika
Mahakamani kufuatilia mashauri yanayoendeshwa ili waweze kuwa na taarifa za
kutosha pindi shauri linapofunguliwa na kutolewa hukumu ili kuwawezesha wananchi
kupata taarifa za kutosha za mwenendo wa Mashauri.
Aliongeza
kuwa Mahakama ya Tanzania imedhamiria kufanya
kazi na waandishi wa habari nchini kwa kuzingatia kwamba wakati majaji wanapotoa
hukumu mahakamani kunakuwa na idadi ndogo ya wananchi wanaoshuhudia kuliko ile
iliyo nje ila vyombo vya habari kutokana na umuhimu wake huwapasha habari mamilioni
ya watanzania walio nje ya Mahakama.
Alisema Mahakama
itaendelea kujenga mahusiano mazuri na Vyombo vya Habari hususan waandishi wa
Habari za Mahakama kwa kutenga maeneo ndani ya Mahakama yatakayotumiwa na
waandishi hao kuwawezesha kufanya kazi zao bila vikwazo kwa mujibu wa sheria,
kanuni na taratibu zilizopo.
Pia alieleza
kuwa Mahakama, itaendelea kutoa taarifa za ufafanuzi wa hukumu mbalimbali
zitakazotolewa kwa vyombo vya habari pia Nakala za taarifa za Hukumu kwa
waandishi wa habari ili kuwawezesha wananchi kujua ukweli wa yale yanayojili
mahakamani kuondoa upotoshaji unaotokea.
Aidha
alisema kuwa Mahakama itaendelea kushirikiana
na Baraza la Habari Tanzania (MCT) katika kutoa mafunzo ya kuwajengea
uwezo waandishi wa habari za Mahakama ili waweze kuandika habari zenye ukweli
na uhakika.
Mhe. Shaban
Lila alisema kuwa Mahakama iko tayari kupokea maoni yanayohusu utendaji kazi wake
ili iweze kuyafanyia kazi kwa manufaa ya vyombo vya habari na wananchi.
Awali akizungumza na washiriki wa mafunzo hayo kabla ya kumkaribisha
Jaji Kiongozi kufunga mafunzo hayo, Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala Mahakama ya
Tanzania Bi. Wanyenda Kuta aliwaambia washiriki wa mafunzo hayo kuwa Mahakama inaendelea kutekeleza
nguzo 3 ambazo ni kuhakikisha kuwa kunakuwa na Upatikanaji wa Haki kwa Wakati,
Kuongeza Imani wanachi kwa Mahakama pia kuboresha miundombinu ya Mahakama
nchini.
Alisema
kuwa wandishi wa Habari za mahakama waliohudhuria mafunzo hayo yaliyoandalia na
Mahakama ya Tanzania na Baraza la Habari Tanzania (MCT) wamejifunza masuala
mbalimbali ambayo yamewajengea ufahamu waandishi wa Habari za Mahakama kuhusu
lugha za kimahakama, uandishi bora wa habari za Mahakama, Uhuru wa Mahakama
pamoja na kujua Haki za Washitakiwa na Watuhumiwa wanapofikishwa mahakamani.
Kwa
upande wake Meneja wa Maadili wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) Allan Lawa
akizungumza na wanahabari hao aliwataka waandike habari za Mahakama kwa
usahihi na umakini mkubwa kufuatia Mafunzo
waliyoyapata.
Bw. Lawa aliishukuru
Mahakama mafunzo hayo na hatua ya uongozi wa mahakama kuyakubali mapendekezo yaliyotolewa na
Waandishi wa Habari za Mahakama ikiwemo kutenga eneo ndani ya mahakama
litakalotumiwa na waandishi wa Habari za Mahakama, utoaji wa Nakala za kesi na
ufafanuzi wake mara hukumu zinapotolewa, Mahakama kukubali kushawishi
uanzishaji wa madawati ya Habari za Mahakama kwenye vyombo vya Habari pamoja na
mahakama kukubali kuendesha mafunzo ya mara kwa mara kwa waandishi wa Habari za
Mahakama na wahariri wao.
Post a Comment